Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 




TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com

TVT Wapiga debe wa CCM


Mmoja wa watangazaji katika TV inayojiita ya Taifa akisoma kile wanachokiita HABARI. Itakumbukwa kwamba wakati maelfu ya watanzania walikuwa wakifa kwa njaa na magonjwa, Redio Tanzania ilikuwa ikiwatangazia watanzania wasihofu kwani uchumi wa dunia nzima umeharibika kuliko wa Tanzania. Wanahabari walopaswa kuelimisha jamii wanapoipotosha wanabaki kuwa mazuzu. Sijui majumbani mwao huwaambia nini jamii zao. Kwamba wanalipwa na Serrikali kuuficha ukweli? Je wakikutana na wanataaluma wenzao hawaoni haya kusema wanafanya TVT? Labda wawe hawana dhamiri zinazowahukumu. Lakini watajilaumu maishani. Baada ya kupewa visenti kidogo na serikali, bado maisha yanawashinda. Wengi wao huvalishwa suti kazini ili waonekane nadhifu, lakini hali halisi ni kinyume. Usishangae kukutana nao uwasahau. Wanatumiwa lakini kwa kiwango duni sana. Je taaluma ya uandishi wa habari inauzwa bei rahisi hivyo? Wengine sifa za kuonekana kwenye TV zinawatosha. Hawajali wanaonekana wakisema nini, kwani hata wasemayo siyo wao walioyaandika. Wameandikiwa nao husoma kama KASUKU. Kwamba mtu atasoma mpaka chuo kikuu na kugeuzwa KASUKU, hilo ndilo linalotisha. Kwa nini kupoteza muda huo shuleni kama hawaruhusiwi kufikiri na kusema waliyoyafikiri? Ni watu wazima tena wasomi. Kwa nini kila mtu asiruhusiwe kubeba lawama na pongezi za kazi yake. TVT ni Mungu? Hata iwaamulie nini cha kusema? Mungu mwenyewe amewapa uhuru wa kufikiri na kusema. Mbona uhuru huo uchukuliwe na TVT na wanahabari wala hilo haliwasumbui? Bora kuuza nyanya sokoni kuliko kuajiriwa TVT au RTD. Muuza nyanya analo la kujivunia. Yuko huru kimawazo. Japo haruhusiwi kuyatoa mawazo hayo kwenye vyombo vya habari, lakini furaha ya kuwa huru kimawazo na kusema anayoyaamini japo kwa watu wawili, inatosha kuiona sababu ya kuishi. Wanahabari wengi maisha kwao ni mateso. Hawafikiri, na wale wanaofikiri hawaruhusiwi kuyatoa mawazo yao. Mbaya zaidi wako kwenye vyombo vya habari. Ni sawa na kumuweka samaki majini na kumzuia asinywe maji. Siyo ajabu wengi hufa kabla ya wakati wao. Wanaoishi huishi maisha yasiyotimiza lengo. Ajabu ni kwamba, wenyewe hawalioni hilo. Hujidai kwamba wanafanya kazi katika TV ya Taifa. Kila la kheri katika kazi yaop hiyo. Ninayeandika haya ni mwandishi wa kuzaliwa, lakini hata nilipwe dola milioni moja kwa mwezi, siwezi kukubali kuajiriwa na TVT na RTD pamoja na magazeti ya Uhuru na Mzalendo. Ndiyo sitokubali kuajiriwa DAILY NEWS. Sababu muulize Mkapa mwandishi wa habari aliyekuwa Rais na kuzifungia kazi za wasanii hata wale wa injili. Kosa lao ni kuimba kwamba CCM imezeeka. Kwa serikali ya Tanzania hayo ni matamshi ya kuharibu amani. Yaani amani ni pale kila msanii na mwandishi anaposema mawazo ya Nyerere yaliyoshindwa yadumu. Kwao hiyo ndiyo amani ndani ya kisiwa cha umasikini alichokichimba Nyerere akitumia siasa ya UJAMAA ulioshindwa kabisa.

Wanahabari Tanzania, hasa wale wanaofanya kazi katika vyombo habari vya serikali, ni vibaraka wa serikali. Wanaegemea upande wa serikali hata kama serikali husika inakiuka haki za binadamu. Tangu enzi za Nyerere vyombo vya habari Tanzania viligeuzwa kuwa wasemaji wa serikali. Nyerere aliitumia sana redio Tanzania Dar es Salaam kueneza injili yake ya ujamaa na kujitegemea. Matokeo yake yakawa ni kushindwa vibaya kwa siasa ya ujamaa jambo lililopelekea afya ya Nyerere kuzorota na hatimaye kuiaga dunia.Mwalimu wa kila kitu kama Watanzania walivyozoea kumwita,pengine alishindwa kuishi avumilie aibu ya kuwadanganya Watanzania kwa zaidi ya miongo miwili na kuwaacha wakiwa masikini kuliko walivyokuwa wametawaliwa na wakoloni. Uhuru haukuwa kuwawezesha watanzania kujitawala, bali ulimruhusu Nyerere awatawale kwa fimbo ya chuma aliyoiita UJAMAA na kujitegemea. Hata baada ya Nyerere kuacha ulingo wa siasa Tanzania, Hakuna jipya.Bado katiba inasema nchi ni ya ujamaa huku wananchi wakidanganywa kwamba wako huru kuingia katika soko huru kinyume na ujamaa, lakini hawajui waingie kiasi gani kwenye sera za utandawazi. Wengi wanauona huo kama mtego wa serikali, ili wakiwa mabepari serikali kama kawaida yake watumie azimio la Arusha kutaifisha mali za wananchi kama Nyerere alivyofanya na kuwaacha watanzania wengi wakiwa na hofu ya kutafuta mali kwa bidii. Mkapa aliyetumiwa na Nyerere miaka arobaini kuwaosha watanzania bongo zao, alikuja na kuwaambia kwamba sasa wanaweza kuingia katika soko huria bila kuibadili katiba. Yeye Mkapa na CCM pekee ndio waliokuwa wakijua wanamaanisha nini. Ndiyo maana Mkapa leo ni tajiri wa kupindukia wakati watanzania ni masikini wa kutupwa.Alichokosea ni kulitumia gazeti alilotumia kuwaelimisha watanzania kwamba sasa kweli nchi yao haifuati siasa za ujamaa.Kwamba hakuibadili katiba, na sioni wakiibadili karibuni, basi nchi ya Tanzania itabaki kuwa ya ujamaa wa Nyerere ulioshindwa, na sioni siasa hizo zikileta manufaa yeyote kwa watanzania. Suluhisho siyo kulegeza kamba miguuni mwa watanzania na kuwaambia wako huru, bali ni kuwafungua kabisa kutoka kwenye kamba mbaya za ujamaa ulioshindwa. Hilo haliwezekani hadi pale serikali ya CCM itakapokubali kuibadili KATIBA ya Ujamaa iwe katiba ya watanzania kwa ajili yao na siyo CCM. Kama hilo halitafanyika, CCM waendelee kuwandanganya wengine lakini siyo Munishi. Ninaamini kwamba katiba ikibadilishwa, kutakuwepo na kipengele kinachowaruhusu wagombea binafsi, na ndipo nitakapogombea urais Tanzania na kuleta mwamko mpya mbali na ule wa CCM ulioshindwa kabisa.

TVTimerithi utamaduni wa kutangaza propaganda za CCM na kuziita habari kutoka kwa Redio Tanzania. Redio iliyokuwa ikiendeshwa kwa pesa za walipa kodi Tanzania iligeuzwa kuwa kituo cha propaganda za siasa ya ujamaa iliyoshindwa. Wakati maduka Tanzania yalikuwa hayana bidhaa, na watu waliohamishwa makwao kwenda kwenye misitu iliyoitwa vijiji vya ujamaa, Redio Tanzania ilikuwa ikicheza nyimbo za kuwahamasisha watu waende porini. Wengi wakati huo waliliwa na wanyama pori huku vyombo vya habari vikitangaza kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani. Kwa nini wanahabari waliohusika kuudanganya umma wasishitakiwe katika mahakama za kimataifa? Utasema walikuwa kazini. Mwanahabari anaezingatia miiko ya taaluma hiyo, asingekubali kuajiriwa na TVT au Redio Tanzania. Dhamiri yake ingemhukumu wakati akitangaza uongo wa serikali wakati wananchi wanaumizwa na sera mbaya za ujamaa na kujitegemea kumbe hali halisi ilikuwa ujamaa na kugawana umasikini. Sawa na vyombo vya habari Rwanda vilivyotumika kusababisha mauaji ya halaiki, Vya Tanzania vilitumika kusababisha kudumaa kwa bongo za watanzania na itatuchukua zaidi ya miaka mia moja kurekebisha hali hiyo. Japo waliokufa hawakufa kwa mkupuo kama Rwanda, lakini walikufa polepole na wanaendelea kufa isitoshe wataendelea kufa. Tunaamini siku moja haki itatendeka na wahusika wote kuhukumiwa katika mahakama za kimataifa zinazojihusisha na haki za binadamu. Wakati huo ukifika ndipo watangazaji wote wa TVT pamoja na wale wa Redio Tanzania, bila kuwasahau wenzao wa magazeri ya UHURU na MZALLENDO, pamoja na Daily News lililokuwa likihaririwa na Mkapa kabla awe rais, watakapofikishwa mahakamani kujibu kuhusika kwao katika kuyadidimiza maisha ya watanzania na kusababisha vifo vya maelfu ya watanzania. Watakaoepuka ni wale watakaoamua kujiuzulu kazi zao kwa kuiheshimu taaluma ya uandishi habari. Bora kuuza nyanya sokoni kuliko kufanya kazi na TVT au Redio Tanzania. Waandishi waliokaa vyuoni miaka yote hiyo hawana uhuru wa kusema chochote kukihusu chama kinachotawala




Serikali Tanzania huwatapeli wananchi. Huku TV ya Taifa ikiwalisha wananchi mawazo ya kikomunisti kutoka urusi, serikali inawahadaa wananchi kwamba wako huru kuingia katika soko huria. Mawazo ya kikomunisti yako kwenye mifupa ya wanahabari wengi Tanzania. Wengi walipata elimu yao huko Urusi.Redio Tanzania pamoja na TVT bado zinaongozwa na watu wenye mtizamo wa Ujamaa wa Nyerere ulioshindwa. Ni mawazo hayo ndiyo yanayozidi kuwadidimiza watanzania katika dimbwi la umasikini. Inashangaza kwamba TVT watajiunga RUSSIA TV kwa masaa zaidi ya manne kila siku kuwaosha watanzania bongo zao. Pengine ni ukosefu wa vipindi hasa ukilinganisha kwamba bado mitambo yao ni ile iliyopitwa na wakati. Bado wanatumia Real to Real tape jambo ambalo linawaacha maili nyingi nyuma. Lakini bado pesa za walipa kodi hazipaswi kutumika kuharibu bongo zao kwa mawazo yaliyopitwa na wakati ya UKOMUNISTI. Yalimshinda Nyerere sioni yeyote Tanzania akifaulu na ujamaa.

Huwezi kujua sera za kitapeli serikalini mpaka uitizame TVT. Maazimio yote serikalini lazima yasemwe na msemaji wa serikali ambaye ni TVT, RTD, na magazeti ya UHURU na MZALENDO. Vyombo vya habari huwaamuru wananchi watii amri ya serikali, na siyo kuwasilisha malalamiko ya wananchi kwa serikali husika. Utasikia TVT wakisema serikali imewaamuru wananchi Singida wahame kwenye hifadhi za misitu, lakini hutawasikia wakiuliza serikali kwamba wanahama kwa nini? na watakwenda kuishi wapi? Mbaya zaidi watakaojaribu kuuliza, wataitwa majambazi, wavamizi wa misitu, na watu wasiojali mazingira.Tanzania serikali hufanya kila kitu. Wao ndio wanaomiliki ardhi, tena ndio wauzaji wa magazeti, tena wanamiliki redio na TV ambazo kuweka tangazo inabidi uwalipe kiwango kikubwa cha pesa. Mashamba yote makubwa ni mali ya serikali, tena wanachagua yale yenye vianzio vya maji. Wawekezaji ndio wanaoruhusiwa kumiliki ardhi Tanzania kwani wao lazima waingie mikataba na serikali. Walishaumwa na nyoka, hawakubali kuwekeza bila mikataba. Wanajua serikali Tanzania ni matapeli.

Nyerere aliwahi kutaifisha mali za watu akitumia azimio la Arusha. Kile ambacho wananchi hawajakijua ni kwamba bado Ujamaa haujatokomezwa Tanzania. Wananchi kwa sababu ya elimu duni, hawazijui haki zao. Bado wananchi wanahamishwa makwao, kwa kisingizio cha kuhifadhi mazingira. Ardhi yote Tanzania ni mali ya serikali. Wananchi ni watumwa wa serikali bila kujua. Wanaothubutu kuingia msituni na kuanza kulima, hujikuta wakiitwa wavamizi katika nchi yao. Nchi ya Tanzania ni kubwa sana na kila mwananchi anaweza kujikimu kimaisha kama serikali ingewaruhusu kumiliki mashamba. Ujamaa ulioshindwa ulikuwa ukisema udongo wote Tanzania ni mali ya serikali. Hawajaukana ujamaa.

Serikali imeona iwafanye watanzania watumwa wake kwa siri. Wanatumikishwa bila kujua na faida yote inakwenda serikalini. CCM na viongozi wake ndio mabwana wakubwa, na wananchi ni watumwa. Hata wale wanaojidanganya kufanya biashara, bado ni watumwa, kwa maana serikali huamua kuwatoza kiwango kikubwa cha kodi.

Nani awasaidie wananchi kama siyo vyombo vya habari? Nani awaelimishe kama siyo hawa wahuni wanaojiita wanahabari huku wakilamba miguu ya viongozi wa CCM? Historia itawahukumu. Tanzania ni ya watanzania na siyo mali serikali ya CCM na viongozi wake. Tuna haki ya kuifikisha serikali mahakamani pamoja na vibaraka wake vyombo vya habari vinavyochangia kumomonyoka kwa maisha ya watanzania.

TVT waache mara moja kutumiwa kuwanyanyasa wananchi, na badala yake waheshimu miiko ya taaluma ya uandishi habari. Badala iwe ni serikali inawaambia wananchi wafanye nini, Watanzania waruhusiwe kutumia vyombo vya habari kuiambia serikali iwafanyie nini. Kama serikali ndio kila kitu, basi wawafanyie wananchi kila kitu. Vinginevyo wawaruhusu kumiliki ardhi ya kutosha na waruhusiwe kufanya biashara bila bugdha ya serikali.

Kile serikali inachokiita hifadhi ya misitu, ni kuwasumbua wananchi bure. Hakuna sababu ya kuwa na hekari za mraba Zaidi ya mia nne elfu 400,000 Singida na kuziita hifadhi ya wanyama pori, huku wananchi na mifugo yao wakikosa malisho. Lazima tufikie mahali pa kujiuliza, ni nani wa muhimu Tanzania? wanyama pori? au watanzania? Mungu ametupa nchi ya Tanzania tuitawale pamoja na wanyama pori wawe chini yetu. Siyo sisi tuanze kuwaabudu wanyama pori kuliko wananchi wa Tanzania.

Hata watalii sijui ni wangapi wanaotembelea Singida na Mbeya kuona kile serikali inachokiita hifadhi. Kikwete aache MKWALA wa kujifanya anatunza mazingira. Huwezi kutunza mazingira ya wanyama pori kabla ya kutunza mzingira ya wanadamu ambao ni wananchi wa Tanzania. Bora wanyama pori waishe tukose dola kidogo ambazo huishia kwenye mifuko ya viongozi wa CCM, kuliko kuwatesa wananchi kwa kisingizio cha kutunza wanyama pori.

Pia ni lazima wananchi wafikie mahali pa kutangaza vita na wanyama pori pamoja na serikali ambayo haitofautiani na wanyama hao wa porini. Tena tunatakiwa tuelimike kiasi cha kuwatimua wanahabari wanaotumiwa na serikali kuja kuwachukua picha waonyeshe mateso yenu bila kuwasaidia. Hiyo ni kuwadhalilisha kijinsia na waandishi kama hao wanaweza chukuliwa hatua za kisheria katika mahakama za kimataifa.


Vijana msipoamka usingizini, CCM itaitawala Tanzania mpaka nanyi mzeeke mkingoja kesho isiyofika.Mnajua kwa nini watanzania badala ya kusema wahudumiwe madukani au sehemu mbali mbali za biashara wao husema NAOMBA. Unaweza danganyika ufikiri ni lugha ya heshima. Hapana. Ni lugha iliyozaliwa baada ya sera za Nyerere kuiharibu Tanzania kiasi kwamba bidhaa muhimu ziliadimika madukani. Sukari ilikuwa ikipatikana kwa mgao. Soda kwa ajili ya sherehe za harusi ilibidi upate kibali cha mkuu wa mkoa ili uweze kununua soda kreti mbili. Kila kitu ilibidi upewe kibali aidha na balozi wa nyumba kumi au mkuu wa wilaya au Nyerere mwenyewe. Ilifikia mahali watanzania waliokamatwa na sabuni za kuogea kutoka Kenya, walijikuta jela sawa na kukamatwa na madawa ya kulevya. Maduka yalikuwa tupu bila bidhaa. Ukiwa na pesa zisingekusaidia wakati huo. Ilibidi UOMBE uuziwe sukari, uombe uuziwe mchele, uombe uuziwe petroli, na kadhalika. Lugha ya KUOMBA ikazaliwa. Hadi leo watanzania ni omba omba. Wanaomba kila kitu. Usishangae wanaume wakiomba kuwachapa wake zao wanapowakosea. Yaani mke wangu umenikosea Naomba nikuchape. Naye mke aombe kukubali kuchapwa. Halafu mume Aombe tena kuanza kumchapa. Muda unapotea na hawa watu hawajaanza kuchapana ndipo wafanye shughuli nyingine. Umasikini ukaivamia Tanzania kama ukoma. Nyerere akawadanganya wasijali mambo yako hivyo kila mahali. Akawaambia wawe wajamaa. Yaani hakuna mtu mwenye chake Tanzania. Unapika ugali kwako na mboga unachukua kwa jirani. Tanzania ikawa ndiyo nchi pekee unaweza kumaliza mwaka bila kununua chumvi. Utaipata kwa jirani, ya nini kununua? Walishindwa kujiuliza huyu jirani anayenunua chumvi ya kuwagawia majirani atafanya hivyo mpaka lini kabla naye afilisike? Mwisho wajamaa wakawa hawana cha kushirikiana ila umasikini. Vyombo vya habari vikatangaza kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani na upendo watu wasio na haraka kwani serikali na majirani zako watafanya kila kitu kwa ajili yako. Wazembe na wazururaji walipozidi, Nyerere akaanza zoezi la kuwakamata. Sera zake ndizo zilizowaaribu, na sasa anawakamata kwa kisingizio cha NGUVU KAZI. Mpaka leo watanzania hawaoni kwa nini wafanye kazi kwa bidii katika nchi ambayo majirani wanakusomeshea hata watoto, wanakulipia bili za umeme, wanakupa simu upige bila kununua salio, na kadhalika. Hata TUT waliohubiri injili hiyo hawaoni sababu ya kwenda na wakati katika kutayarisha vipindi. Wakishaisifia CCM na Kikwete, wananyoosha miguu, eti wamemaliza kazi ya uandishi wa habari


CCM ndio waliochangia kuyafikisha maisha yetu yalipo, na ndio wanaozidi kutunyanyasa. Hatuwataki, tumewakataa, na hatuwakubali. Imetosha. Sasa basi. Liwalo na liwe.Nani waliotuambia serikali ya ujamaa itatufanyia kila kitu? ni CCM. Nani waliouza mashirika yetu kwa wageni? ni CCM. Nani wanaotukamata kwa sababu ya kufanya biashara ndogo nchini mwetu? ni CCM. Nani walioharibu mambomba ya maji safi ili makampuni ya wakubwa yatuuzie maji? ni CCM. Nani wanaocheka tunaposhindwa kununua maji safi na kupatwa na KIPINDUPINDU? ni CCM. Nani wanaotutangazia kwamba tuchemshe maji kabla ya kunywa huku wakijua wazi maji safi hayapatikani? ni CCM. Bado mnawataka wawatawale? HAPANAAA!!!!!

Dhana ya watanzania kujenga utamaduni wa kutotilia maanani ELIMU ilijengwa na vyombo vya habari. Redio tanzania na TVT hutangaza kwamba wanafunzi wa darasa la saba wamemaliza shule. Halafu wale wachache wanaochaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, hawaitwi waliohitimu, bali waliochaguliwa na serikali ili waje wawe vibaraka wa serikali katika nyadhifa ambazo wenyewe hawakuzichagua. Yaani mfumo wa elimu Tanzania huingiliwa kisiasa. Serikali kwa makusudi huwaacha watanzania wakiwa mbumbumbu kielimu na kuwatangazia kwamba wamemaliza shule. Kwao kuwatawala watu wasio na elimu ni rahisi. Ndio maana wale waliomaliza shule wakifanya kile wanachokijua wanajikuta jela. Wamachinga wote ni wale waliomaliza shule Tanzania. Wakati dunia nzima inasema elimu haina mwisho, Serikali ya CCM hujigamba kwamba kila mwaka wanafunzi wa darasa la saba humaliza shule. Wanapoamua kujiajiri wenyewe kama wamachinga, Serikali hiyo hiyo inawakamata na kuharibu biashara zao. Wakiuliza kulikoni, wanaambiwa wangoje kesho.

 
| http://munishi.com |