

TV ya INJILI Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM
Tel.
254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com
Aibu
Yaifunika Tanzania







Serikali ya Mkapa imefanya kosa la kiistoria pale ilipowafukuza waandishi
wa habari wa nchi jirani ya Kenya. Waliyataka wenyewe, na yalipokuja
sasa wanayakimbia. Baada ya gazeti la "Mwananchi' kuuzwa kwa
kampuni ya 'NATION", Wakenya waliwekeza mabilioni ya dola za
Kimarekani katika sekta ya habari na utangazaji nchini Tanzania. Kile
ambacho hawakukijua, ni kwamba sekta hiyo haijawahi kuwa huru Tanzania.
Walipoanza kuandika habari kulingana na taaluma yao, gazeti la 'Mwananchi'
lilianza kuchanja mbuga Tanzania, na kuwa moja kati ya magazeti yanayoongoza
nchini humo. Serikali ikaliona hilo. Kama kawaida yao kuthibiti habari,
walijaribu kulitumia gazeti la 'Mwananchi" liwapigie debe CCM
wakati huu wa uchaguzi. Inasemekana wanataaluma hao waliikatalia serikali
usoni, jambo lililosababisha kutimuliwa kwao. Mkapa ameithihirishia
dunia kile ambacho walikuwa wakikijua tayari. Kwamba Tanzania hakuna
uhuru wa kutoa mawazo. Na kwamba utitiri wa vyombo vya habari Tanzania
ni kifunga macho ili jumuia ya kimataifa ione kwamba kuna uhuru wa
habari, kumbe asilimia 99 ya vyombo hivyo humilikiwa na serikali pamoja
na maajenti wake. Inasemekana Mkapa mwenyewe anamiliki zaidi ya magazeti
8 yakiwemo yale ya kidini ambayo hayaachi kuweka picha yake mbele.
Anapomaliza urais na kuirudia kazi yake ya uandishi, Mkapa atakumbukwa
kama mwanahabari aliyepata madaraka yakamlevya, kisha akaanza kuwatesa
wanahabri wenzake.

Umewahi kujiuliza kwa nini
mabalozi wa Tanzania nchi za nje karibu wote ni wanajeshi wastaafu?
Je Serikali huwatumia kufanya ukachero kwenye nchi hizo? Au hujihusisha
na mambo ya kidiplomasia kama yalivyo? Je wanajeshi na wanadiplomasia
ni taaluma moja? Kwa nini Serikali zote tangu Nyerere zimekuwa zikifuata
desturi hiyo? Je ni mbinu ya kuwatawanya wanajeshi ili wasiweke vichwa
pamoja kuitoa serikali dhalimu ya CCM? Hayo na mengine mengi, Mwandishi
wetu atayaangalia katika makala haya.
Serikali za awamu tatu Tanzania
zimekuwa zikiendeshwa kihuni. Wananchi wanatishwa ili wasitoe maoni
yao.Vyombo vya dola Polisi, Usalama wa Taifa, Uhamiaji pamoja na vikosi
vya siri vimekuwa vikifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba
CCM inaendelea kubaki madarakani. Mengi hufanywa kwa siri sana, kiasi
kwamba ukiwa nje ya Tanzania huwezi kuamini kwamba CCM na Serikali
zake wanaendesha mambo kihuni. Pengine nakosa neno sawia na matendo
ya CCM. Ukiwaita wahuni haitoshi. Ni wauaji, Tena washirikina wa kiwango
cha juu sana. Pia nikiwaita wezi haitoshi kulingana namna wanavyofanya
wizi wao. Pengine Majambazi Matapeli litakaribia sifa yao. Je mtu
anayekuibia na huna pa kumpeleka anaitwaje? Hao ndio CCM. Kwa sababu
ya kuendesha mambo kinguvunguvu, wanajeshi huwa wanawafaa sana. Ndiyo
maana katika utawala wa CCM wamekuwa wakitumia wanajeshi kuliko raia.Nyerere
alijua kwamba Wanajeshi ni amri. Tena wanajeshi wana nidhamu. Isitoshe
Wanajeshi hutii halafu maswali baadaye kama watakuwa hai kuyauliza.
Ni sababu hizo na nyingine ndizo zilizomfanya Nyerere kuwatumia wanajeshi
katika utawala. Alilazimisha wasomi wote kwanza wapitie mafunzo ya
Kijeshi kuwakamua kiburi cha usomi. Mpaka leo kamba alizosuka Nyerere
hazijakatwa, kwani awamu zote zimekuwa zikifuata mfumo wa Nyerere
aliyeanzisha ujamaa ukashindwa.Nyerere aliwafundisha wanasiasa Tanzania
jinsi ya kuiba chakula na kupangusa mdomo. Wanaiba, Wanaua, Wanaharibu
nchi kwa sera mbovu, Lakini utashangaa Kimataifa Tanzania inahesabika
kama kisiwa cha amani wakati si kweli. Ni mpaka mtu mwenye mawazo
huru aingie Tanzania hata kama ni mwezi mmoja, Halafu ajaribu kujieleza
kwa Watanzania, Ndipo atakapogundua kwamba Tanzania ni nchi tofauti
kuhusiana na haki za kibinadamu. Uaskari askari uko kwa kila mtu.
Upeo wa kimawazo unafuata mkondo mmoja. Yaani Tanzania iko Ki-Nyerere
Nyerere vile. Wanasiasa Tanzania ni sawa vinyonga. Utawaona wapole
kumbe ni wezi wakubwa. Hakuna mtu anaeyajua haya nisemayo kama kampuni
ya magazeti ya Nation. Walitapeliwa wakauziwa gazeti lililokuwa la
chama na Serikali "Mwananchi" Waliponunua na kuanza kufanya
kazi ya uandishi kitaaluma, ndipo walipoanza kuuona upande wa pili
wa Serikali. "Mwananchi" lilianzishwa 2000 kuelekea uchaguzi
mkuu. CCM walilitumia gazeti hilo kwa propaganda. Wafanyikazi karibu
wote walikuwa maofisa usalama wa Taifa. Hatujui kama "NATION"
walipoinunua kampuni hiyo wafanyikazi wa zamani walibaki. Kama walibaki,
"NATION" watajidanganya kusema magazeti yao Tanzania yatakuwa
huru mbali na kuingiliwa na Serikali. Wakijaribu kufanya hivyo, Wataiona
nguvu kubwa ya CCM ambayo huwa imejificha. Lakini kama "NATION"
na kampuni yao mpya "Mwananchi" wataendelea na ujasiri wao
wa kufichua mambo, Basi Tanzania itakuwa siyo sehemu nzuri kufanya
hivyo. Ni nchi yangu naijua. Nawajua wanasiasa wa Tanzania wanavyoitumia
dola kulinda maslahi yao maovu. Sikushangaa niliposoma kwenye "NATION"
kwamba Serikali Tanzania ina mpango wa kuwatimua wanahabari wa Kenya.
Serkali ya Tanzania inaongozwa na wahuni. Usipounga mkono maovu yao,
basi watakufanya chochote. Watatumia kila chombo cha dola. Idara ya
UHAMIAJI ikiwa mojawapo. Ni
kawaida yao. Wamezoea. Na hawapelekwi kokote. Kinachoniumiza moyo,
ni mabilioni ya shilingi za Kenya "NATION walizotapeliwa na Serikali
ya Tanzania. Kwamba sasa wanawatimua, Mtu anaweza jiuliza kwa nini
waliwauzia kampuni hiyo ya "MANANCHI" ikiwa kuwapa vibali
ni vigumu? Hata kama
wewe ni Mtanzania usishangae kuitwa mkimbizi kutoka Zambia. Wana habari
wa "NATION" wako Tanzania kufanya kazi kulingana na taaluma
yao na siyo kuipigia debe CCM. Kama Mkapa alifikiri kwamba "NATION"
ni "UHURU" na "MZALENDO" magazeti ya chama, atakiona
kilichomnyima kuku kutoa maziwa anyonyeshe vifaranga. Namshukuru Mungu
kwamba "NATION" wamejionea wenyewe yale ambayo nimekuwa
nikiyalalamikia kwa miaka mingi. Kanda yangu ilipigwa marufuku kwa
kusema "CCM aliyoanzisha Nyerere imezeeka, Sijui "MWANANCHI"
walisema nini. Lakini Wahuni wa DAR, wameanza fujo zao. Safari hii
wameuma kubwa kuliko uwezo wao kutafuna. Pengine wateme. Wakimeza
itawakwama kooni.Jipeni moyo "NATION" Mungu ni mkuu kuliko
CCM na Mkapa mwanahabari anaewatesa wanahabari.Wengine wanasema pengine
ni baada ya gazeti la 'Mwananchi' kuandika makala kumhusu Munishi
Rais mtarajiwa Tanzania ndipo gazeti hilo likajipata matatani. Kuna
wale wanaosema hiyo siyo sababu kwani gazeti hilo pia liliwahi kuandika
kumhusu Komba anayejikomba na CCM. Lakini iwe ilivyokuwa tayari Tanzania
imejifunua uchi mbele ya dunia ionekane inavyovikandamiza vyombo vya
habari.
Gazeti
la "MWANANCHI" Lasema:
Gazeti
la "MWANANCHI"
Walichokosea ni kutosema kwamba Munishi nitagombea Urais Tanzania.
Nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania bado iko pale pale.Kwamba katiba
hairuhusu wagombea binafsi, hiyo hainifanyi nijiunge na chama chochote
cha kisiasa ili nitimize masharti ya KATIBA. Kwangu siasa ni uongo,
na siwezi kujiunga na uongo niwatoe waongo. Ikiwa CCM hawataibadili
Katiba iruhusu wagombea binafsi, basi tutaiasi katiba tuandike yetu.
Wakichaguana nasi tutachaguana. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa
KATIBA ya Injili na serikali ya Injili, Rais wa Injili na Bunge la
kiinjili. Hapo ndipo tunapoelekea. Siyo
ajabu kwani tayari tuna nyimbo za GOSPEL kilichokuwa kimebaki ni KATIBA
ya Gospel Itakayounda tume ya Gospel ya uchaguzi utakaomchagua Rais
wa Gospel atakayeunda Serikali ya Gospel akitumia wabunge wa Gospel.
Waislamu wakiona vyema wajiunge na Gospel tutawakaribisha. Wakiona
waunde yao ya SHARIA, ni sawa. Pia kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa
nchi ya serikali zaidi ya kumi. nayote hayo yatafanyika kwa amani.
Kikwazo cha amani Tanzania kitakuwa ni CCM pale watakapokataa mabadiliko,
na kungangania madaraka.Kama kawaida yao wataanza kuwalaumu wengine.
Lakini wananchi safari hii wameerevuka na wanamjua mbaya wao ni nani.CCM
ndiye nyoka anayestahili kupondwa kichwa.


