Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 



GOSPELGTV.COM


TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com

Msafara wa Moi ajalini


Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Daniel Toroitich Moi, akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye ajali iliyohusisha msafara wake, lakini gari iliyogongwa ni ile iliyokuwa imembeba yeye.Maswali mengi yameulizwa, lakini majibu yake yatatoka kwa mkuu wa Polisi. Iweje gari iliyombeba RAIS igongwe wakati zile za walinzi ndizo zilizopaswa kugongwa zikimlinda RAIS? Je lilikuwa jaribio la kuyakatiza maisha ya Moi? Kibaki Rais wa sasa Kenya analionaje hilo? Marekebisho gani serikali itayafanya katika kikosi kinachomlinda Rais wa zamani? Kuna mtu atakayefutwa kazi kufuatia ajali hiyo?


Siyo kwamba Rais Kibaki anamcheka mwenzake, inasemekana alikuwa akimpa pole.Wote wawili sasa ni marais waliowahi kuhusika katika ajali mbaya barabarani. Kibaki alipata ajali alipokuwa hajawa Rais, wakati Moi ameipata akiwa rais mstaafu.Ilikuwa hivi. Msafara wa Moi ulikuwa ukielekea Nakuru. Walipofika kinungi, gari aina ya pick up Datsun iligongana na Land cruiser iliyombeba Moi. Walinzi wa Moi walimrudisha Nairobi na baada ya kufanyiwa uchunguzi Nairobi Hospital, aliruhusiwa kwenda nyumbani. Haijulikani kama alienda Kabarak au alipumzika kwenye nyumba yake Nairobi. Lakini TV zote zilimuonyesha Moi akitoka Hospitalini, japo alikuwa akichechemea kidogo. Kesho yake habari ikageuka kwamba alirudishwa Hospitalini masaa machache baada ya kuruhusiwa. Walisema kwamba madaktari walionelea wamfanyie upasuaji wa goti ambalo lilionekana kuumizwa na pigizo la ajali. Pia walisema itambidi Moi akae hospitalini hapo, kufanyiwa uchunguzi zaidi.

 
| http://munishi.com |