Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 




TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com

Polisi Kenya wamuua Matheri

Polisi nchini Kenya wamemuua kwa kumpiga risasi kisogoni Matheri waliyemwita Jambazi sugu na hatari. Pichani ni Matheri kabla na baada ya kuuawa. Pamoja naye ni mwanamke ambaye hakuweza kujulikana jina lake. Aliuawa pamoja na Matheri. Inaonekana kwamba Polisi walimfunga mikono nyuma kabla ya kumuua nje kidogo ya nyumba yake baada ya kujisalimisha.
Walifanya shambulio hilo usiku wa manane nyumbani kwa Mtuhumiwa huyo, baada ya kujisalimisha kulingana na mkewe.Akionge na camera za TV baada ya tukio, Mkewe Matheri alisema kwamba Polisi waliizingira nyumba yao na kumwamuru Matheri ajisalimishe au waichome moto nyumba yao. Baada ya Polisi walibadili tishio lao na kusema wangeimiminia nyumba yote risasi kupitia madirishani. Ndipo mke wa Matheri alipomsihi ajisalimishe ili awanusuru watoto na Matheri alikubali bila swali. Aliongeza kwamba baada ya kuhojiana na polisi huko nje kwa zaidi ya nusu saa, mama huyo alisikia kukurupushani na baadaye milio ya risasi jambo lililomuashiria kwamba mume wake awezakuwa amejeruhiwa vibaya au awe amekufa.

Hawa ni mke na watoto wa marehemu aliyebandikwa jina la Jambazi sugu Kenya. Inawezekana kuna ukweli fulani katika tuhuma hizo, lakini kwa hawa watoto Matheri alikuwa baba aliyekuwa anakutana na mahitaji yao. Wapiga picha wetu walikuta mabaki ya chapati na kitoweo cha nyama ya kuku jambo linaloashiria kwamba Matheri alikula chakula cha jioni na jamii yake, asijue Polisi watauchukua uhai wake usiku huo.
INdivyo ilivyo hakuna aijuae siku wala saa ya kuja kwake Yesu mwana wa Mungu. Ndiyo maana tunawaonya majambazi wote watubu na waziache njia zao mbaya kwani wasipofanya hivyo hakuna wa kuwarekebisha kwani hata Polisi wameamua kupoteza ubinadamu nao wanafanya kama majambazi wafanyavyo. Majambazi wanaua na Polisi wanaua. Tofauti yao ni gani?

Hata NDOVU hawezi kuwindwa na Polisi wengi hivi. Lakini nani hasa aliyeamua kwamba ni heri kuyamaliza maisha ya Matheri kuliko kumpeleka gerezani akaone TV na kucheza mpira baada ya makamu wa Rais Mudy Awori kuyafanyia ukarabati magereza ya Kenya. Je sasa sheria za utaratibu wa mahakama umewachosha Polisi wetu kufikia kuamua kuwaua wahalifu hata pale wanapojisalimisha?
Dunia hii ya Mungu tutaona Mengi kabla Yesu kurudi. Wanyama wa porini hawana sheria wala mahakama. Kuuana na kuchinjana ni mtindo wa maisha mazima mwituni. Lakini kuna ndege ambao huwa hawapendi kuona damu ikimwagika kila siku. wanachofanya ni kupiga kelele wanapowaona simba wakilikaribia kundi la swala. Wakisikia maonyo wanakimbia kabla wakutwe. Wakipuuza shauri yao watajilaumu wenyewe. Nasi tumechoshwa na umwagikaji wa damu kila siku kila mahali duniani. Tunachofanya hapa ni kupiga kelele ili wanadamu wote waukimbilie usalama kwa Mungu wao. Vinginevyo shetatani amewaingia wanadamu na wanafanya kama wanyama. Ubinadamu umewatoka. Kimbieni kwa Mungu kwa njia ya kutubu dhambi na kumwamini Yesu ili dhambi zenu zisamehewe na majina yenu yaandikwe kwenye kitabu cha uzima.


Mzazi wa Matheri baada ya kuburuzwa chumba cha maiti kuutambua mwili wa mwanae. Inasemekana hakuongea. Haijalishi walimwita nani, lakini kwake ni mwanae, na uchungu wa mwana aujuae ni mzazi.
Kila mzazi hajui anazaa nini. Rais karani, Daktari wote huzaliwa. Hakuna anayependa kuzaa jambazi. Lakini ikitokea uwe ulizaa jambazi kosa hapo linakuwa la nani? Mbona nasikia mzee huyu amepokea kipigo kutoka majirani mara nyingi na hata wamemchomea nyumba? iweje makosa ya mtoto aathibiwe mzazi? tena bila kuufuata mkondo wa sheria? Tulichokiona asubuhi ya kuuawa kwake huyo waliyemwita jambazi mkuu Kenya, hakikufurahisha, kinatisha na hakipaswi kurudiwa. Jamii ikikosa mwelekeo ianze kufurahia mauaji ni kinyume na amri za Mungu. Kuua ni kazi ya Mungu na hakuna mwanadamu anayeruhusiwa kufanya hivyo kwa sababu zozote. Akitokea mwanadamu aliyepotoka kiasi cha kuondokewa na ubinadamu wake aanze kuua, wale walio na ubinadamu bado wanapaswa kufanya kila linalowezekana kumrudisha huyu aliyepotoka katika maadili sahihi ya ubinadamu. Kuua haijawahi kuwa suluhisho. Tena haiwezi kuwa adhabu maana kila mtu atakufa. Utamwadhibuje mtu kwa kile kitakachokupata hata bila kufanya kosa? Bunduki na mlio wake mkali haijawahi kutatua matatizo duniani. Tena haitawahi wala msitegemee kwamba siku moja mtutu wa bunduki utamaliza ujambazi duniani. Kitendo cha polisi kummiminia risasi Matheri baada ya kujisalimisha na kisha kumburuza baba yake mzazi akaione maiti ya mwanae, hicho hakikuwa kitendo cha kibinadamu. Tunakilaani kwa nguvu zetu zote. Hakuna mtu anayeunga mkono ujambazi. Pia hatuifurahii kazi ya majambazi. Polisi wanaposema Matheri ndiye jambazi nambari wani Kenya, wanapaswa kuthibitisha hilo. La sivyo Matheri atabaki kuwa mtuhumiwa wa ujambazi aliyeuawa baada ya kujisalimisha kwa Polisi. Kitendo hiki kitaichonganisha jamii na Polisi kuliko na majambazi. Sababu7 ni kwamba Matheri wanayesema aliua, hatukumuona akiua, lakini tumewaona Polisi wakimuua. Kwa watoto wa Matheri waliowashuhudia Polisi wakimmiminia risasi baba yao, Kwao haitafutika kwamba Polisi ni wauaji.Inasemekana kwamba mkewe Matheri alimtaka ajisalimishe ili kumnusuru yeye na watoto, jambo ambalo Matheri alikubali bila swali. Hii inaonyesha huyo waliyemwita Jambazi hatari, alikubali kujitolea kwa polisi kuepusha waliokuwa wakiitafuta roho yake wasiwadhuru watoto. Je baada ya kumuua Matheri haki itawahi tendewa wanaodaiwa kuuawa na Matheri? Je Ujambazi Kenya utamalizika na wakenya walale milango wazi? Hayo ndiyo maswali polisi walipaswajiuliza kabla ya kufyatua risasi kumwelekezea Matheri na mwanamke wanayedai alikuwa msaidizi wake. Na kweli Polisi haikuona umuhimu wa kumwacha hai huyo mwanamke awasaidie kuwakamata majambazi wengine? Kama wote wawili walijisalimisha kama magazeti yote Kenya yalivyoripoti, kwa nini kuwaua? Katika suala hili tunawapongeza Media kwa kufanya kazi nzuri. Panapokosekana Polisi na Mahakamazinazofuata maadili ya kazi yao, isikosekane Media inayoripoti ukweli kama ulivyo hata kama wengine hawataufurahia. Mbona Polisi walimkamata mkewe Matheri baada ya kuwasimulia wanamedia kwamba mumewe aliuawa baada ya kujisalimisha? Je walitaka story hiyo iripotiwe vinginevyo? Kwa upande wao Polisi walimhusisha Matheri na mauaji Mengi nchini Kenya, yakiwemo yale ya Wamarekani wawili waliouawa karibuni mjini Nairobi. Nao Amerika wamesisitiza kuendelea na uchunguzi wao kuhusu kilichosababisha mauaji ya raia wao, huku wakikataa kuamini kwamba yalisababishwa na Matheri kama Polisi wanavyodai. Kuna wanaoamini kwamba kusakwa na hatimaye kuuawa kwa Matheri kulichangiwa sana na mauaji wa Wamarekani na siyo vita halisi ya ujambazi unaowasumbua Wakenya. Picha nyingine inayopatikana katika sakata hili ni kwamba Polisi wanawajua majambazi wote, na mmoja anakuwa hatari wakati anapotofautiana na baadhi yao katika mgao. Ni siri iliyo wazi kwamba visa vingi vya ujambazi Afrika vinahusisha baadhi ya wana vikosi vya usalama. Kuna wanaodai kwamba Polisi wakiwania kumaliza ujambazi inawezekana kama wataanzia na wao wenyewe. Lakini mambo yalivyo sasa ni kwamba kila jambazi anapaswa kujiuliza mara mbili kabla ya kushirikiana na polisi kufanya ujambazi. Mambo yakienda mrama usulubishwe, hata kama utajisalimiosha itabidi shaba iingie mwilini mwako ili usiwaseme maofisa unaoshirikiana nao. Je ukweli huu utafichwa kwa muda gani? Tunashukuru kwamba Media Nchini Kenya wameanza kuchimbua kuelekea kuupata ukweli unaofichwa mara nyingi katika watuhumiwa wanaouawa baada ya kujisalimisha. Sambamba na hilo tunalaani kwa nguvu zote watu wanaoacha kufanya kazi kwa jasho lao na kujihusisha na vitendo vya ujambazi. Mbaya zaidi wanawaua wanaowaibia mali zao. Huo siyo ubinadamu. Watu kama hao wanapaswa kuibadili mienendo yao na kufanya kazi kwa mikono yao wajipatie riziki badala ya kuwa majambazi. Majambazi wakifanya makosa na Polisi wafanye makosa, Media wakisema ukweli wakuu wa dini tunapaswa kuwapongeza wakweli. Katika hili tunawapongeza Media Nchini Kenya na tunawataka wengine barani Afrika waige mfano wao mzuri.

 
| http://munishi.com |