![]() ![]() |
||
BBC gospel TV gospelradio Gospel radio gospelnews Gospel
news |
Msitu mpya
Nyoka ni wale wale CITIZEN nao hawakuachwa mfukoni bali walitoka na kuanza kuonyesha habari hizo japo baadaye walionyesha kutokuwa na moto nazo sana. Lakini ukweli unabaki kwamba Vyombo vya habari viliungana kupinga uvamizi huo kwa nguvu zote , jambo lililopelekea viongozi na wananchi kuwaunga mkono bila kujiuliza maswali mengi. Hiyo ndiyo nguvu ya MEDIA. Kushawishi.Lakini mara nyingi wanakosea na wanaweza kushawishi vibaya. Swali ni nani wa kuwauliza? Wenyewe wanahabari wanadai kwamba hawaulizwi kitu na mtu yeyote ila wana uwezo wa kujiuliza wenyewe. Wanasema kwamba wanafuata sheria katika kutekeleza kazi zao, na wangetarajia Serikali nayo ifuate sheria katika kuwavamia wanapoandika UONGO. Mkufunzi mmoja katika chuo kikuu kimoja humu nchini, Aliwashangaza Wakenya pale aliposema kwamba sheria za Kenya haziwazuii wanahabari kusema UONGO, labda wakiwa kwenye kiapo. Aliendelea kusema kwamba hata kama story iliyozua utata ilikuwa ya UONGO, Serikali ingenyamaza kimya kwani sheria inawaruhusu wanahabari kusema UONGO. Alizifanya nywele zangu zisimame pale aliposema kwamba "UONGO umekatazwa kwenye amri kumi za Mungu na mtu pekee kuwahukumu wanahabari waongo ni Mungu." Aliitaka Serikali iwaachilie mara moja wanahabari wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuandika habari za UONGO kuhusu mkutano wa siri kati ya Kibaki na Kalonzo. Alidai kwamba hakuna kipengee cha sheria cha kuwashitaki hata kama wamesema UONGO. Alimaliza kwa kusema MUNGU pekee ndioye anayeweza kutoa ushahidi dhidi yao na kwa kuwa Mungu hawezi kuja mahakamani nchini Kenya kutoa ushahidi, basi serikali inajisumbua kuwapeleka wanahabari hao mahakamani.Hayo yalisemwa kwenye TV ya NTV asubuhi ya kuamkia uvamizi wa polisi kwenye magazeti ya STANDARD na KTN pamoja na kuchomwa moto magazeti yote ya siku hiyo ya kampuni ya STANDARD. Aliyekuwa akiyasema hayo ni mkufunzi katika chu kikuu, na kazi yake ni kuwafundisha wanahabari. Aliyekuwa akimhoji ni "DADA" Mukami sijui kama ameolewa au la, Usisahau wanahabari hawaulizwi chochote kuhusiana na maisha yao. Wanakosoa hawakosolewi. Hilo ndilo linalonisumbua. Mkufunzi alipoulizwa mbona gazeti la STANDARD lilikataa kufuata agizo la Serikali la kuwataka waombe msamaha na kuandika story ya kukanusha UONGO wao. Mkufunzi wa wanahabari
anasema hakuna mtu mwenye haki ya kuwaamuru wanahabari nini waandike
na nini wasiandike. Kwa matamshi hayo wanahabari ni wa pili kutoka
Mungu. Hawaogopi chochote wala yeyote hata serikali hawaiogopi. Wanasema
Serikali ya Kibaki itaondoka na wao watabaki wakiwa wanahabari. Wana
KIBURI kuliko Michuki aliyeifananisha serikali na nyoka. CNN wakimjibu
Michuki walisema badala serikali iwe ndiyo itakayouma, itaumwa. Kwa
maneno mengine, waligeuza maneno ya Michuki na kuyafanya yaonekane
kwamba nyoka siyo serikali bali nyoka ni wanahabari. Kwangu suala
la kujifananisha na nyoka mwenye sumu linanikera. Ndiyo maana nimechukua
kalamu na karatasi na kuanza kuandika. Usijali kama nilikaa chuo kikuu
chochote na kufundishwa kusema UONGO kama wanahabari, Lakini lengo
langu ni kuchukua fimbo ya karibu niue nyoka. Nitamponda kichwa kabla ya nyoka kunigonga kisigino. Nyoka ni nyoka. Awe na sumu au la ni nyoka. Serikali haipaswi kujifananisha na nyoka. Sambamba na hilo waandishi wa habari hawapaswi kuwa na KIBURI kiasi cha kuwaona wengine katika jamii hawafai kuwakosoa. Hatuwezi kuukataa ukoloni tuukubali ukoloni wa kutawaliwa na vyombo vya habari. Uchungu wa kutawaliwa unafanana. Haijalishi nani anayekutawala, Lakini kutawaliwa na vyombo vya habari ni kubaya zaidi. Wanatawala mawazo yako kiasi kwamba hutawahi kuwaza kujikomboa. Sijui utaniita nani, lakini sipendi majivuno na KIBURI wanachoonyesha wanahabari. Wanasema wanapigania haki ya kutoa mawazo na uhuru wa kusema, huku wakiwanyima wengine haki hiyo. Wanasema wanaimulika serikali kuhusiana na RUSHWA, huku wenyewe wakiwa wala rushwa nambari moja. Unafiki huu ndio nitakaouponda kichwa. Wanahabari wanajifanya kujua kumkosoa kila mtu lakini wenyewe hawapendi kukosolewa. Niliimba wimbo wa INJILI na ndani yake kukawa na maneno ya kusema nawaombea wanahabari waache kupokea rushwa kutoka kwa wanasiasa. Media zote ni kama zimeupiga marufuku wimbo huo. Hauchezwi popote. Kisa? Wanahabari hawaambiwi chochote na yeyote. Nani aliyewadanganya kwamba wao watachukua nafasi ya Mungu duniani? Kama wanavyopenda kukosoa, wakubali kukosolewa. Vinginevyo wakiwa na KIBURI waseme kwamba wana haki ya kusema uongo, basi wajue nasi tuna haki ya kuwakataa waongo kwa nguvu zote hata kama itabidi kutumia polisi wafanye uvamizi kama uliofanywa STANDARD na KTN. Wanadai hakuna sheria inayowakataza kusema UONGO. Pia wasisahau kwamba hakuna sheria inayowakataza polisi kuingia NTV usiku na kuwauliza nyimbo za INJILI wanazocheza kwenye vipindi vya dini wamepokea rushwa kiasi gani? Watazamaji hudanganyika kwamba wanasikiza nyimbo za GOSPEL. Kumbe wenye maduka makubwa ya muziki huwalipa wanahabari ili nyimbo walizonunua kutoka kwa wasanii zichezwe kila mara. Usijali kama wasanii husika hulipwa sawa na sanaa yao, Lakini mapato ya kazi zao huishia mifukoni mwa wenye maduka pamoja na wanahabari. Je hiyo siyo RUSHWA ambayo Githongo anapaswa kurudi Kenya anase sauti ya wanahabari wakipokea rushwa kutoka duka moja Nairobi lijulikanalo kama NDUTI ONE STOP? NTV bila haya huwadanganya watazamaji wake kwamba nyimbo za INJILI Kenya ni zile zinazomilikiwa na NDUTI ONE STOP SHOP. Huo ni mfano mmoja kama tone la maji kwenye bahari. Media karibu zote zimeoza kwa RUSHWA na hawataki kuambiwa hivyo. Wanapokataa kucheza wimbo wangu unaowakemea, ni sawa na Serikali ilipowavamia kwa kuwakosoa kuhusu RUSHWA, ambayo wenyewe wanaikumbatia. Kama kawaida yao watasema Munishi ana usongo na wao. Kwa nini niwe na usongo na wanahabari ambao nami ni mmoja wao? Wangetakiwa wakubali kukosolewa nami, kuliko kungoja "MAKOMANDOO usiku. Ni siri iliyo wazi kwamba taaluma ya wanahabari imevamiwa na rushwa kila kona. Tunajua wanafanya biashara halali. Tunachowaomba ni kwamba habari ziwe ni habari na siyo mbinu za kutangaza kampuni au biashara fulani baada ya kupokea RUSHWA. Waweke wazi nini kinauzwa na nini hakiuzwi. Tunajua wazi kwamba matangazo ya biashara ndiyo pekee yanayopaswa kulipiwa. Siku hizi kila nafasi katika Media inauzwa. Ukiona habari ukurasa wa mbele wa gazeti, au usikie wimbo fulani kila siku kwenye redio, mwite Githongo achukue vifaa vyake vya kazi, halafu tafuta mwanahabari aliyehusika kuucheza wimbo au kuandika habari hiyo, Kisha fuatilia nyendo zake, Utamuona akiingia kwenye duka la NDUTI ONE STOP SHOP, na kukutana na mmiliki wa duka hilo na kisha kupokea RUSHWA. Usiwaite polisi wamkamate, ngoja kidogo. Mfuatilie akirudi NTV, KAMEME FM, HOPE FM, BIBLIA HUSEMA FM, INORO FM, ni karibu zote. Kisha uone anagawana na nani pesa hizo. Sasa waite polisi wavamie kituo hicho. Utashangaa kuona maofisa wa vyeo vya juu katika majumba ya habari ndio wahusika wakuu wa RUSHWA. Zamani ilikuwa ni MADJ, ikagundulika kwamba DJ anampita mkubwa wake kazini kimapato. Walipogundua kwamba DJs wanapokea RUSHWA, hawakuizuia rushwa kwenye vyombo vya habari, bali walitafuta mbinu za knufaika nayo. Sheria kali zilitungwa kuhakikisha DJs hawachezi wimbo ambao mkubwa ameukubali. Ikatoka kwenye kitu kidogo wimbo ulie, mpaka kwenye donge nono ili wagawane na mkubwa. Ilikuwa aibu kwa msimamizi wa stesheni kumuomba pesa za "LUNCH" mdogo wake kikazi au DJ. Walipogundua wapi pesa zinatoka, wakabuni mbinu za kuzichota. Wasanii binafsi walipigwa marufuku kupeleka nyimbo zao kwenye Media, na badala yake makampuni makubwa ya kimuziki ndiyo yanayopewa kipaumbela. Kwa nyimbo za HIP HOP Gospel na zile za dansi, wanaoongoza ni "Ogopa DJs" Msanii akikubali kuwauzia nyimbo zake, kwanza anapewa hakikisho la kujulikana kwani nyimbo zake zitalia kila mahali. Usijali nani atakaefaidika baada ya kujulikana huko. Msanii anabaki na jina kubwa bila pesa, makampuni ya muziki na wanahabari wanapata pesa. Tunapotetea haki za wasanii tutatumia chombo gani kufanya hivyo wakati Media zote zinashiriki katika kuwanyanyasa wasanii? KBC Shirika la utangazaji Kenya walijaribu miaka ya themanini kuinua vipawa vya wasanii hasa wa nyimbo za INJILI, lakini jitihada zao zimekwamishwa na utitiri wa vyombo vya habari ambavyo vinatilia maanani pesa kuliko kujenga sanaa ya Kenya au Afrika kwa ujumla. Kwa kutumia vipindi kama JOY BRINGER na SING AND SHINE, KBC walikuwa wa kwanza kuonyesha kazi za wasanii bure bila kuwatoza chochote. Matokeo yake yalikuwa kuwajenga wasanii wabunifu ambao walijua ubora wa sanaa yao ndio utakaowafanya waonekane kwenye TV au wasikike kwenye redio. Siku hizi mambo ni kinyume kabisa. Rushwa ndiyo itakayofanya wimbo wako usikike na kuonekana NTV. Usijali kama sanaa katika wimbo huo ni ya kiwango gani, lakini kama wanahabari wamechotewa, utausikia wimbo huo kila siku mpaka uamue kuzima NTV uende Channel nyingine. Omba Mungu ukute huko nako hawana kipindi cha Muziki. Usishangae kuukuta wimbo huo ukicheza TV zote na redio zote. Na bado habari za wimbo huo zitaandikwa magazeti yote. Ukiona hivyo jua wanahabari wanaojifanya kupambana na Rushwa serikalini wamekula RUSHWA. Sasa mambo yakiwa hivyo zoezi la kumaliza RUSHWA liko mbali kuanza wachilia mbali kumalizika. Wanahabari walio katika nafasi nzuri kukemea Rushwa na wenyewe ni wagonjwa. Munishi akisema wanamwita "kontrovashio." Ukiwaita waongo wanasema uongo ni sehemu ya kazi yao. Wakivamiwa usiku ili uongo wao uchomwe kabla ya kuwaharibu raia wema wawe waongo, wanasema wameonewa. Ukiwaambia waseme kweli, wanasema hakuna vipimo halisi vya kupima Ukweli na uongo. Ukiwaambia Neno la Mungu ni kipimo tosha, wanasema Mungu hawezi kuja mahakamani kutoa ushahidi. Wana habari ni watu wa ajabu sana. Wengi wao hawajaoa wala kuolewa lakini ndio washauri wa ndoa za wasomaji na wasikilizaji wao. Ni watumiaji kupita kiasi, usishangae wana kipindi cha kuwafundisha jamii jinsi ya kubana matumizi. Wanavaa wapendavyo, lakini wao ndio wanaoandika kwamba tabia za mtu huonekana kwenye mavazi anayovaa. Kichwa kinaniuma. Wanashauri kila mtu lakini hawashauriwi. Wanamshambulia
mzee Michuki na kuonyesha matundu katika soksi za mzee wasijue ni
laana kuonyesha uchi wa babu kama Michuki hadharani. Sasa wanataka
mzee wa watu ajiuzulu. Kosa lake ni kuwaambia walisema uongo. Kwamba
nimeandika na umesoma, niite upendavyo. Ukiamua kuniita mwandishi
wa habari, ujue mimi kusema uongo siyo sehemu ya uandishi wangu. Pengine
ni kwa sababu sijafunzwa na mkufunzi yeyote anayedai kusema uongo
ni sehemu ya kazi ya uanahabari. Naomba kutofautiana naye katika hilo
na asinielewe vibaya.
|
||||||||||||
|
|
|
|