

TV ya INJILI Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM
Tel.
254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com
James
Kim Apokonywa mchumba

Baada ya kujitafutia mchumba, walipanga siku ya kufunga pingu za maisha.
Kabla ya kujuana kimwili, James alimuona mchumba wake akiwa na mimba.
Tofauti na ile ya bikira Maria iliyokuwa kwa uwezo wa roho Mtakatifu,
Hii ya mchumba wa James ilikuwa kwa uwezo wa Pastor "MWENYE ROHO
MTAKAVITU". Pamoja na jitihada za Pastor huyo kumtaka Kim amuoe
msichana huyo, inasemekana kwamba juhudi hizo zimegonga mwamba kwani
James Kim amekataa kata kata.Ndoano iliyotumika kumnasa binti huyo
ni "Huyo Kim ana nini? Tafuta nyumba Buru Buru na kama unataka
sana kumuona huyo Kim wako, basi nitamwajiri awe mlinzi wa usiku kwenye
hiyo nyumba" Hayo ndiyo maneno yaliyommaliza nguvu mchumba wa
Kim. Na kweli inasadikiwa kwamba msichana huyo amekodishiwa nyumba
kwenye mtaa wa Buru Buru mjini Nairobi, Lakini kim ameikataa kazi
ya WATCHMAN huko. Mengi zaidi muulize James kim Mwenyewe kwenye simu
ya mkononi +254723552655
Kanda
Mpya


Mwinjilisti James Kim amechomoa kanda mpya. James aliyekuwa mchezaji
hodari wa vyombo katika huduma ya Mchungaji James Maina Nganga. Inasemekana
kanda yake hiyo, imeanza kupata umaarufu katika Kanisa la Neno Evangelisim.
Muda mfupi baada ya kanda hiyo kutoka, uhusiano wake na Pastor ulianza
kuzorota, jambo lililopelekea kusimamishwa huduma mara moja. Kwa sasa
hana masoko ya kuiuza kanda yake kwani alitegemea kanisani ambako
alihudumu kungekuwa soko la kwanza kabla ya wengine kuijua kanda yake.
Akiwa katika Ofisi za Gospel GTV, alituonyesha barua aliyopewa kusitisha
huduma yake kanisani hapo.




Inaonekana kuna vita baridi kati ya waimbaji na wachungaji. Wachungaji
wakiona huduma za waimbaji zinaaza kushamiri, wanaanza mbinu za kuwamaliza
kihuduma. Hatuungi mkono utovu wa nidhamu kati ya baadhi ya waimbaji,
Pia sambamba na hilo, Hatuwaungi mkono Wachungaji wenye wivu. Matatizo
ya waimbaji mengi wamejiletea wenyewe, Lakini ni kweli kwamba wachungaji
nao wanachangia pakubwa kuwadidimiza waimbaji. Katika ukurasa huu
kumejaa visa vya waimbaji walioteswa mikononi mwa wachungaji wenye
wivu na wengine tabia zao haziambatani kabisa na maandiko matakatifu.
Hii imeendelea kujenga ukuta mkubwa kati ya waimbaji na Wachungaji.
Hakuna sababu ya Mchungaji kuwasakama Waimbaji kwa sababu tu wametoa
kanda ili wajitegemee. Kuna ubaya gani kufanya hivyo? Waimbaji wengi
hufanya huduma zao makanisani kwa misingi ya kujitolea na siyo vibaya
wakijikwamua kiuchumi wakitumia sanaa yao.Wengi hawalipwi, na kama
wanalipwa ni kidogo sana kuwawezesha kumudu mahitaji ya kila siku.
Kuwatumia waimbaji halafu uwatupe unapofanikiwa kihuduma, ni sawa
na kuwaua. Hiyo haimpendezi Mungu hata kidogo.Mapato ya makanisa mengi
huishia mifukoni mwa wachungaji wakati waimbaji huambiwa wamtumikie
Mungu. Kwani kuna kosa gani kwa muimbaji kumtumikia Mungu huku akitumia
sanaa yake kujilisha na kujivisha? Je Wachungaji wanapotumia vibaya
pesa za kanisa kwa anasa, Nani awape barua ya kuachishwa kazi? Wengine
hudai kwamba wao wameitwa na Mungu kwa hiyo wana haki ya kutumia pesa
za kanisa wapendavyo. Siyo kweli.Kanisa ni washirika pamoja na Pastor.
Bila washirika kusingekuwepo na pesa ambazo Wachungaji hujivuna nazo
Redio
za Injili na Wanamuziki wa Gospel
.


Mwinjilisti Kim akifikiri kazi imeisha, Alijikuta ndio kibarua kinaanza.
Alirauka asubuhi kuanza kuzitembelea Redio Stesheni ili ziweze angaa
kucheza nyimbo zake ziweze kujulikana. Hakuyaamini masikio yake pale
alipoambiwa wazi kwamba lazima atoe kitu ndipo nyimbo zake ziweze
kusikika. Kwa kijana ambaye ameachishwa kazi na kupewa Elfu tano ambazo
alilipia nyumba zote, kumwambia atoe pesa ndipo nyimbo zake ziwekwe
hewani , ni sawa na kumtuma James Kim maziwa ya kuku na sijui atayapata
wapi. Baada ya kutoka KBC ambako walichukua CD yake bila kuahidi wataicheza
lini, Kim alienda Redio CITIZEN ambako nao pia walimpokea vizuri na
kuichukua CD yake. Lakini alipofika kwenye redio ya Injili BHB ambako
alitegemea kukaribishwa vizuri kuliko alikotoka, Huko Biblia husema
aliambiwa lazima alipe shilingi elfu mbili ndipo nyimbo zake zichezwe.
Alipouliza kama atapewa risiti ya pesa hizo isiwe kwamba anatoa rushwa,
Alijibiwa kwamba risiti ataipata. Ilimbidi Kim azunguke mguu na njia
ili kuweza kupata Kshs.2000. Mungu alikuwa mwema kwake kwani msamaria
mwema aliamua kumsaidia baada ya kuelezewa magumu aliyopitia Kim.
Alirudi haraka BHB na kuwalipa, na siku hiyo hiyo walianza kuucheza
wimbo wake ambao kila anayeusikia anabarikiwa rohoni. Kweli safari
ya WOKOVU ina mengi njiani.
Hapa ni risiti
Kim aliyopewa BHB baada ya kukataliwa katakata kwamba nyimbo zake
haziwezi kuchezwa bure.
Mwinjilisti James Kimwele.
Mungu akikugusa kumsaidia kijana huyu, Fanya hivyo kwa kutumia simu
yake +254723552655 Ni mchezaji mzuri wa gitaa, na karibu nyimbo zote
alizowahi kuimba mchungaji Nganga kijana huyu ndiye hucharaza Lead
Gitaa au Bass.Pia anajua kucheza piano vizuri sana.
Jiandikishe
Hapa
Hata
kuishi Amerika ni haki yako


