Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 


 

 

 

 



TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com



Kikwete Ameanza wizi
Anaendeleza mbinu za Nyerere kuwatisha raia

Hawa ndio wanajeshi wa Tanzania. Tumbo kubwa ndio mtindo jeshini. Inasemekana mkuu wa majeshi ana ndege zake binafsi. Katika nchi ambayo wanasiasa hushirikiana na Polisi kuwapora wananchi mali,Mtu anaweza jiuliza kwa nini wanajeshi nao wasipate sehemu yao ya mlo? Tangu Kikwete aingie madarakani inaonekana ameamua kuwapa wanajeshi mlo wa kiaina yake. Amebuni kikosi kinachojumuisha wanajeshi na wanausalama wa Taifa kuwasumbua raia mitaani. Wana amri ya SHOOT AND KILL. Kuua kwao siyo jambo kubwa mradi kisingizio kiwe aliyeuawa ni jambazi hatari. Tofauti na polisi wa kawaida, hawa rushwa yao huchukua kwa beseni na siyo sahani. Yaani ukitaka kuwahonga uanzie mamilioni. Wanajiita SUPER SWEEPER. Wanafyagia mali kutoka kwa yeyote anayeonekana mpizani na kuikabithi mali hiyo kwa Kikwete mwenyewe akiimarishe chama.

Ukitaka kujua kitakachokupata ukiipinga CCM muulize DR. Lamwai. Alisukumwa kushoto kulia na kitambo ajue nini kinaendelea, alijikuta akiwa masikini wa kutupwa. Hadi alipoamua kurudi CCM na kumsifia Kikwete kwa umaarufu wake wa kutembea na wake za watu ndipo angalau aliruhusiwa kufnya kazi nchini Tanzania. Yaani ukiwa mpinzani wa kweli, utabanwa kiasi cha kushindwa kupumua. Lamwai alipomwambia Kikwete ni sawa kuvunja ndoa ya waziri wake wa mambo ya nje, Ndipo aliporudishwa zizini.

Alichosahau kumwambia ni kwamba dini ya Kikwete inamruhusu kuoa zaidi ya wake wawili. Haikuwepo sababu ya Kikwete kuvunja ndoa ya mtu. Vinginevyo angetafuta binti wa kitanzania au nje ya Tanzania amuoe awe mke wa pili au wa tatu, hata wa nne akitaka. Uislamu dini ya Kikwete unaruhusu hilo.Nasikia kwamba Lamwai ndiye anayemshauri Kikwete amtayarishe huyo mwanamke awe mgombea urais Tanzania baada ya Kikwete. Hatupingi nchi ya Tanzania kuongozwa na mwanamke, lakini siyo lazima awe kimada wa Kikwete, tena aliyemuacha mumewe bila sababu za msingi.

Akimpokea waziri wa mambo ya nje Tanzania Mrs AshaRoce migiro, Rais Kikwete alimuomba Profesa migiro msamaha. Alimtaja bwana Migiro kama mtu mwenye uvumilivu ambaye tangu mkewe awe waziri wa mambbo ya nje, amekuwa akilala nje. Siyo kwamba analala nje ya Dar es Salaam tu, bali nje ya nchi. Na sasa amechaguliwa kuwa Kaimu wa katibu mkuu umoja wa mataifa, uvumilivu utahitajika zaidi.Ni ukweli usopingika kwamba mwanamke wa kiafrika akishapata cheo kikubwa kiasi hicho, utii kwa mumewe unakuwa ni jambo nadra sana kupatikana. Tunaomba isiwe hivyo kwa Asha. Uzee ndio huo unamnyemelea, kwa hiyo akimuacha Profesa sioni akipata bahati ya kumpata mume wa kuheshimiwa kama bwana Migiro. Kulikuwepo uvumi kwamba Asha alipanga kumuacha Profesa, na kisa kikawa walikuwa wakila uroda na rais wa nchi mheshimiwa Kikwete. Kwamba Kikwete amemuomba msamaha mbele ya watanzania wote hiyo inathibitisha kwamba LISEMWALO kama halipo liko.


Mbunge wa CCM (viti maalum) Bi Amina Chifupa akanusha kwamba amemuacha mumewe Bwana Mohamed Mpakanjia, na kuwa kimada wa Rais Kikwete. Alisema wanaoeneza uvumi huo wana nia ya kumwaribia ndoa yake. Hii ni kufuatia taarifa ya vyombo vya habari kwamba mbunge huyo sasa ana nguvu kuliko Rais mwenyewe. Cha ajabu ameanza kuwapa tumbo joto hata wabunge wenzake kutoka chama tawala. Usijali kwamba hakuchaguliwa na wananchi, Lakini aliyemteua bungeni alijua kwa nini alifanya hivyo. Pengine ni kwa sababu ya dini yake, au urembo wake, na kuna wale wanaoenda zaidi na kusema ni kwa sababu ya misimamo yake katika masuala ya kijamii.Vyovyote vile, lakini sisi tunasema adui wa adui yako ni rafiki. Kwamba amebainisha kile tulichokuwa tunakijua kwamba viongozi wa CCM ni wauza madawa ya kulevya, kwa hilo tunampongeza. Hata kama kikwete alimteua kwa maslahi yake mengine, alichosahau ni kwamba mwanamke akishakuweka kifuani,anachukua mamlaka yako bila wewe kujua. Sasa Tanzania inaongozwa na wanawake vimada wa rais Kikwete. Hatari yake ni vuta nikuvute itakayosababishwa na maslahi ya kila mmoja wao. Sitoshangaa CCM ikijimaliza yenyewe. Wamelewa madaraka kiasi kwamba kila mwanamke mzuri ni mali ya viongozi wa CCM. Safari hii hata biashara haramu ya madawa ya kulevya CCM ndio nambari wani katika kuiendesha biashara hiyo. Hata pesa za kampeni zao chafu kumbe ni pesa haramu zipatikanazo kwa kuuza "UNGA." Nao viongozi wa CCM wanaohusishwa na tuhuma za kuuza madawa ya kulevya, wamemtaka Kikwete amtimue Bi Chifupa katika bunge, wakidai anatumiwa na wapinzani kukisambaratisha chama. Nasi hapa GTV tunampongeza Bi Amina Chifupa, au Mrs. Amina Mohamed Mpakanjia, Au unaweza kumwita Kiburudisho cha mfalme. Majina yake ni mengi. Wengine wanamwita mpelelezi wa Munishi. Vyovyote sisi tunampongeza kwa kufichua uozo ndani ya CCM na viongozi wake. Hata hiyo kuwa kimada wa Kikwete ni sababu tosha ya kutuonyesha jinsi nchi yetu inavyoongozwa na watu ambao wamekosa maadili. Ikiwa Rais ndiye anayesababisha dhoruba katika ndoa za watu, huo ni mfano gani kwa jamii???

Usijali kama KATIBA ya Tanzania inasemaje kuhusu siasa ya Tanzania. Lakini Rais aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ndiye anayevunja katiba. Marais Tanzania wamekuwa wakiikiuka KATIBA na hakuna wa kuwauliza. Katiba ya Tanzania imejaa ujanja ujanja wa Nyerere kiasi kwamba Kikwete na wenzake waliomtangulia hawaifuati. Sasa nchi inaongozwa kihuni bila kufuata katiba.Tunaposema Katiba ya sasa ivunjwe wengine wanatuita wendawazimu. Katiba haifuatwi, na CCM hawataki tuibadili. Huo unaweza kuuita nini? Katiba inasema wazi kwamba nchi ya Tanzania ni nchi ya UJAMAA na KUJITEGEMEA. Nani anyeweza kusema kwamba sera za Tanzania kwa sasa ni za UJAMAA? Yaani watanzania wanadanganywa kwamba wao ni wajamaa, na wasijiingize kwenye ushindani wa kibiashara kwani serikali itawasaidia kila kitu. Wanachoshangaa ni maisha yanavyozidi kuwa magumu kwao na serikali iliyopaswa kuwasaidia haipo. Viongozi wanajitahidi kuiba mali nyingi za umma iwezekanavyo.

Wanajeshi ambao wangetegemewa kuipindua serikali ya wezi, nao sasa wamejiunga na wanasiasa kuiba. Tena wao ndio kabisa wanatufanya tuogope zaidi. Hivi kweli Tanzania ikivamiwa mfano na Burundi, unategemea wanajeshi wenye vitambi kama wagonjwa wa utapia mlo, wanaweza kuilinda mipaka ya nchi yetu? Hebu angalia picha hapo juu uniambie kama Munishi ambaye sasa yuko msituni, akiamua kuingia Tanzania na vijana wanaotumia mitandao ya kompyuta kurusha makombora ya maneno kama hawa jamaa wajawazito wasiojifungua kama wanaweza kupambana. Uongozi wa Kikwete uliingia dosari tangu alipoingia madarakani.

Miezi mitatu madarakani, Kikwete ameanza kutumia mbinu za Nyerere kuwatisha raia Tanzania. Anawatuhumu wananchi kwamba mali walizo nazo hawakuzipata kihalali. Hii ni mbinu ya Serikali kuhakikisha mali zote Tanzania ziko mikononi mwa watu wanaodhaniwa siyo tishio kwa CCM. Ni zoezi la kisiasa kukiimarisha chama tawala. Kwamba Kikwete anatumia mbinu hizo wakati huu, inashangaza. Nchini Tanzania wenye mali kihalali ni wanachama wa CCM na viongozi wake. Wengine wote hata kama siyo wanachama wa chama chochote cha kisiasa, wakiwa na mali CCM hawalali usingizi. Watatunga mbinu za kuwaita majambazi wakati wenyewe ni majambazi nambari wani.

Kama kweli nia ya Kikwete ni kuwasaka majambazi waliojipatia mali kwa njia zisizo halali, aanze na Mkapa ambaye mali zake zote amejipatia kiudanganyifu. Vinginevyo Kikwete hatakuwa na tofauti na aliyekuwa rais wa kimabavu Tanzania William Mkapa. Wote ni watoto wa Nyerere, haishangazi kuona wakizitumia mbinu zake. Wengi walidhani Kikwete atakuwa tofauti kidogo hasa ukitilia maanani kwamba Nyerere alimteua Mkapa badala ya Kikwete. Inasemekana CCM walikuwa wamempendekeza Kikwete lakini Nyerere kwa sababu zake akaona Mkapa anafaa kuliko Kikwete. Wengine wanasema Nyerere angekuwa hai bado angepinga Kikwete asiwe rais. Kwamba Kikwete anatumia mbinu za Nyerere kutisha raia, ili ajisimike ionekane naye yuko, tatizo liko hapo.

Mkapa aliingia na mbwembwe za ukusanyaji kodi, nazo zikageuzwa kisiasa. Badala ya kuwatoza kodi waliostahili ikawa ni fimbo ya kuwakomoa wapinzani wa CCM. Sasa Kikwete ameingia na mbwembwe za kuwasaka majambazi. Tayari zoezi zima limeshaingia dosari pale mashambulizi yanapolenga wale wanaoonekana kupinga CCM. Siasa za Tanzania zimekuwa zikilenga kuwakomoa wale wanaopinga CCM. Mwenyewe unaweza kutafakari kwamba makabila yanayoonekana kuipinga CCM yameteseka kiasi gani chini ya utawala wa miaka zaidi ya arobaini ya CCM. Wanauawa kama kuku na ukiuliza unaambiwa ni majambazi.

Ikiwa kazi ya rais ni kupambana na majambazi, Polisi watafanya kazi gani. Hatusemi Rais asijihusishe wakati hali ya usalama wa raia na mali zao unapozorota, Lakini Tanzania kiwango cha ujambazi siyo kama serikali inavyotutaka tuamini. Tunajua wazi kwamba serikali inaweza kuwa chochote ikitaka. Hatushangai kusikia ujambazi Tanzania hutekelezwa na vyombo vya dola. Polisi ndio wanaowahangaisha wananchi wakiwapora mali zao. Kikosi cha usalama wa Taifa hutumiwa kukusanya habari za nani ana nini kuhujumu CCM, na afanyiwe nini. Badala wakusanye habari za nani anapanga nini kuharibu usalama wa Taifa, wao wanakusanya habari za kulinda usalama wa CCM. Kwamba pesa za walipa kodi zitatumiwa kulinda maslahi ya chama tawala, utata uko hapo. Kikosi cha Usalama wa Taifa ndicho kinachotumia pesa nyingi za bajeti ya serikali. Kisingizio ni kulinda Taifa, Kumbe wanalinda CCM. Makachero hutumia vifaa vya kisasa kumfuatilia yeyote kwa gharama yeyote, ili mradi wapate habari wanazotafuta. Watanzania wengi hawajui kwamba maongezi yao kwenye simu husikilizwa na maofisa usalama wa Taifa ambao kila asubuhi huwasilisha habari hizo kwa Rais. Siyo ajabu tulipomsikia Kikwete akisema kwamba orodha ya watu wanaofaa kushughulikiwa anayo.

Tangu Nyerere aibadili katiba na kuufanya muda wa rais kuwa miaka kumi, Kila rais Tanzania hutumia miaka miwili kufanya mbwembwe zitakazomfanya aonekane tofauti na wengine. Mwaka wa tatu hutumika kuiba pesa tayari kujiandaa kwa uchaguzi ili arudi miaka mitano ya mwisho. Miaka yote mitano ya mwisho hutumika kuiba kwa mbinu zote ili akiachia madaraka awe na utajiri wa kumtosha mpaka siku ya kuiaga dunia. Hayo tuliyaona kwa Mkapa, na tukadhani Kikwete atakuwa tofauti. Tunasikitika kusema kwamba Kikwete anafuata mkondo huo huo, na mbaya zaidi ameanza kuiba mapema zaidi. Unapowajengea watanzania hofu kwamba majina yao unayo, na tena wakati wowote wanaweza kushikwa wajieleze mali zao walipataje, huo ni wizi tayari. Umewapa polisi mamlaka ya kumsumbua yeyote wanayefikiria kuwa ni tajiri, hata kama jina lake siyo mojawapo ya majina aliyo nayo Kikwete. Kitakachofuata na rushwa kwa sana, kwa wale wasiotaka usumbufu wa polisi. Yote hayo yakitendeka, ni serikali inawaibia wananchi ikitumia mkono wa polisi. Nyerere ndiye aliyeanzisha wizi huo, pale alipowaita wenye mali WUHUJUMU UCHUMI wakati uchumi aliuharibu mwenyewe, kwa sera zake za ujamaa zilizokataa kutekelezeka. Aliiharibu Tanzania kiasi cha watu kutupa mali zao wakihofu kukamatwa na kuwekwa kuzuizini. Aliwafanya watanzania waukumbatie umasikini kwani aliharimisha utajiri na kuufanya kosa ambalo adhabu yake ni kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka. Wale Kikwete anaowatuhumu leo, wengi wao waliwahi kuwekwa kizuizini wakati wa Nyerere, ila wakati huo waliitwa WAHUJUMU WA UCHUMI, na sasa Kikwete anawaita watu waliojipatia mali zao nje ya mtandao wa CCM. Kwa Kikwete watu hao ni hatari sana kwa utawala wake. Hofu yake wasiamue kutumia mali zao kuunga mkono upinzani. Yale tunayoyaona na kuyasikia kutoka kwa Kikwete ni mbinu chafu za kisiasa, zinazolenga kuwaibia watanzania haki yao ya kuamua pamoja na mali zao.

Polisi wanatumiwa kutekeleza mauaji ya kisiasa kwa kisingizio cha kupambana na ujambazi. Tayari Polisi chini ya utawala wa Jakaya Kikwete wameanza kutekeleza oparesheni ya Kikwete ya kuua wale wanaodhaniwa ni majambazi. Kwa sababu jeshi la polisi liko chini ya amiri jeshi mkuu wa majeshi yote yaani Kikwete, Hatutakosea tukisema Kikwete ameanza kuua wapinzani wa chama tawala kwa kisingizio cha kupambana na ujambazi. CCM kirefu chake ni CHAMA CHA MAJAMBAZI. Hatuwezi kupambana na majambazi huku tukiacha chama chao madarakani. Kupambana na ujambazi kwanza ni kukitoa madarakani chama cha majambazi CCM. Halafu tuwakamate majambazi wote tukianzia na William Benjamin Mkapa. Kisha kuwakamata hawa wezi wa kuku itakuwa kazi rahisi.

Tatizo la siasa za Tanzania ni UNYERERE. Hakuna wanasiasa wanaojiamini. Kila mmoja anajitahidi kumwiga Nyerere aliyeshindwa na kukiri hivyo. Mwanasiasa pekee aliyethubutu kutofautiana na Nyerere ni Ali Hassan Mwinyi. Heshima anazopewa Mwinyi ni tofauti kabisa na heshima atakazopewa Mkapa. Mwinyi alijaribu kubuni mbinu za kuwatoa watanzania katika dimbwi la umasikini , ambalo alichimba Nyerere na kuwatumbukiza Watanzania ndani. Badala ya Mkapa kufuata nyayo za Mwinyi, alijaribu kuzifuta ili afuate nyayo za Nyerere ambazo zilifutika kitambo. Naye Kikwete ni kama amechanganyikiwa. Hajui afute nyayo za Mkapa, au azifuate. Anapojaribu kukumbuka nyayo za Nyerere na kujaribu kuzifuata, Anajikuta akiharibu zaidi. Watanzania wanataka vitu vipya na mawazo mapya. Nasikitika kusema CCM hakuna wenye mawazo mapya. Wote wanasema zidumu fikra za aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Kambarage Nyerere. Hawawezi bila mawazo ya Nyerere. Matatizo ya Tanzania yatamalizika pale watakapoumaliza UNYERERE kwenye siasa zake. Inashangaza kuwasikia hata wapinzani kama kina Mrema wakimnukuu Nyerere aliyeshindwa. Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Unyerere umekolea kwenye siasa za Tanzania. Hatutegemei mapya kutoka kwa Kikwete aliyefanywa kiwete na mawazo ya Nyerere. Mungu aisaidie Tanzania impate MKOMBOZI.

Siku moja kabla ya uchaguzi Tanzania
Kikwete alizimia


Walikuwa wakimsikiliza Kikwete kwa makini. Uwanja ni Jangwani jijini Dar. Ilikuwa siku moja kabla ya uchaguzi. Akiwa katikati ya hotuba yake iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja kwenye TV na Redio Tanzania, Kikwete aliomba maji. Kabla ayafikishe mdomoni, magoti yalililegea na kuuacha mwili wa Kikwete kupigiza chini kama nyani aliyekosakosa tawi. Mkapa na walinzi wa kikwete walipigwa na butwaa kiasi cha kubaki midomo wazi. Umati ulionekana kuchanganyikiwa wasijue cha kufanya.

Walinzi walikurupuka kumkimbilia Kikwete ambaye tayari alikuwa chini. Waliwaamuru wapiga picha waelekeze kamera zao kwa wananchi wakihofia kwamba Rais mtarajiwa ameiaga dunia. ITV kibaraka wa CCM walikatiza matangazo yao. TVT TV ya Propaganda za CCM nayo haikuwa na jinsi ila kuwatangazia watazamaji kwamba Kikwete alikuwa mzima na wasiwe na wasi wasi. Bila kujua kwamba matamshi hayo ndiyo yaliyowapa watanzania wasiwasi.

Hata Kikwete alipoongea masaa mawili baadaye, watu hawakuamini ni yeye. Ndiyo maana wana CCM wengi hawakujitokeza kupiga kura wakihofu watakuwa wakichagua kivuli na siyo Kikwete. Kwa sasa mtizamo wa Watanzania ni kwenye AFYA ya Kikwete. Je ni mgonjwa kama ilivyodhaniwa?

Mengi yamesemwa kuhusu afya ya Kikwete, lakini baada ya kuzimia hadharani ni dhahiri kwamba uvumi utaongezeka. Siyo kwamba kuwa mgonjwa ni jambo lisilo la kawaida kwa wanadamu, lakini kwa wanasiasa wa Tanzania kuwa wagonjwa ni ajabu. Chukulia mfano wa Kikwete kuzimia na vyombo vya habari kukatazwa kuchukua picha za Kikwete akiwa chini na povu mdomoni. Kwao ni aibu kuchukua picha ya masihi wa CCM akiwa mgonjwa.

Fikiria kwamba kwenye viti vya mbele alikuwepo Mkapa mwandishi wa habari kitaaluma, lakini hata yeye hakuweza kuichukua picha ya Kikwete akiwa amezimia. Pengine hata hakuwa na kamera ya kufanya hivyo. Au na yeye alizuiwa na walinzi kuchukua picha ya Kikwete aliyekuwa amegeuza macho kuwa rangi nyeupe? Ama tuseme walichukua picha na kisha wakakatazwa kuzichapisha.

Je hiyo itamaliza uvumi? au ndio itauongeza uvumi? Hii inaonyesha wazi jinsi Tanzania isivyo na uhuru wa vyombo vya habari. Kwenye mkutano wa CCM iliyoitawala Tanzania kwa zaidi ya miaka arobaini, habari ni nini kama si kuzimia kwa Kikwete? Na habari hiyo ilipojitokeza ulimwengu ulinyimwa haki ya kuhabarishwa nini kilichoendelea hapo. Ikiwa Yesu alisulubiwa msalabani na watu hata wapita njia wakamuona, Kikwete ni nani tukatazwe kuiona picha yake akiwa amezimia?

Hata kama kuanguka kwake kungeambatana na kujisaidia haja zote hapo hapo, bado siyo sababu tosha kuwanyima watanzania waliokuwa wakitizama TV zao haki ya kujua kulikoni. Kufanya hivyo kumejenga hisia kwamba wanasiasa siyo watu wa kawaida. Hawaugui, hawazimii kisha wakajikojolea, au kujisaidia haja kubwa nguoni, Tena miguu ilemewa na kuwiliwili cha wanasiasa walionenepa kwa wizi wa pesa za umma, halafu miguu hiyo ilegee na kumwacha mtu kama Kikwete apigize chini kama gunia la chumvi, eti wanahabari hawaruhusiwi kuichukua picha hiyo?

Kwangu hilo linanisumbua sana. Nijuavyo ni kwamba wanasiasa ni watu wa kawaida kabisa. Wanaugua magonjwa yote hata ukimwi. Kutufanya tuamini kwamba watu kama kina Mkapa na Kikwete ni nusu miungu ni makosa.

Laiti wangeruhusu watu waone picha ya Kikwete akianguka chini alipozimia, hiyo ingezima uvumi ulioenea na unaoendelea kusambaa kwamba Bwana Kikwete ni MHADHIRIKA. Nchini Tanzania wagonjwa wa UKIMWI wanaitwa WAADHIRIKA. Siyo kwamba Ukimwi ni tofauti na magonjwa mengine, Tena siyo ajabu ugonjwa huo kumpata yeyote, lakini wanasiasa wa Tanzania watakuwa wa mwisho kukubali kwamba wanaumwa mafua, achilia mbali Ukimwi.

Fikiria jinsi Kikwete waliyekataa picha yake isichukuliwe alipozimia, Lakini masaa mawili baadaye aliwaita waandishi wa Habari nyumbani kwake akiwataka wamchukue picha akiwa ameoga na sabuni ya OMO kuondoa madoa yote mwilini ili aonekane akiongea kwenye TV zilizozimwa alipozimia. Pamoja na kujitahidi kujikakamua, bado alionekana mgonjwa. Alivyojaribu kutabasamu, ndivyo uso ulivyozidi kukunjamana kwa uchungu. Na alichosema ni kwamba yeye ni mzima wa afya na afya yake haina tatizo lolote. Mtu anaweza jiuliza yote hayo ya nini? Mbona Kikwete ajitetee kuhusu afya yake? Kwani afya yake ina nini?

Anasahau Nyerere alikuwa na afya yake nzuri miaka yote hadi tuliposikia amepelekwa ngambo kutibiwa? Je Nyerere alipopelekwa nje ya nchi kutibiwa ndio ulikuwa mwanzo wa kudhoofika kwa afya yake? Jibu ni hapana. Nyerere alikuwa mgonjwa miaka mingi. Usiri wa kuficha magonjwa huumbuliwa na kifo au kuzimia hadharani.

Sisi katika GOSPELGTV.COM hatuamini kwamba Kikwete ana UKIMWI. Hatuna vipimo vya kuthibitisha hilo. Tunalosema hapa ni kwamba Kikwete ni mwanadamu anaeweza kuugua ugonjwa wowote. Tunamuombea Mungu Kikwete awe na afya njema na kama ni mgojwa Mungu amponye. Lakini mgonjwa anaposema ni mzima hata daktari hawezi kumpa vidonge.

Kwa hiyo wanaoeneza uvumi kwamba Kikwete ni mgonjwa wanasaidiwa na dhana potovu ya serikali kujaribu kuudanganya umma kwamba wanasiasa hawaugui. Serikali na vyombo vyake watakapokubali kwamba watu kama kina Mkapa na Kikwete wanaweza kuzimia mkutanoni na wakubali wananchi waone hilo, ndipo kuugua kwa wanasiasa kutakapochukuliwa ni kawaida na hakutamshitua yeyote.

Lakini hali ilivyo sasa tunamngoja Kikwete aje atuambie kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki, wakati waandishi wa habari walinyimwa uhuru wa kuzichukua picha zake alipozimia. Tena tunasubiri kwa hamu tumsikie Kikwete aliyezinduka aje atuambie Tanzania ni kisiwa cha amani wakati watanzania walinyimwa uhuru wa kuuona picha za Kikwete akibebwa akiwa amezimia. Kama kawaida yake, Safari hii atakuja na cheti kutoka VCT kuonyesha kwamba hana virusi. Hatutashangaa atakapowataka wanahabari wasogeze kamera zao karibu ili tuonyeshwe maandishi yanayosema Kikwete HIV Test ="NEGATIVE" Haijalishi Kikwete atajitahidi namna gani asizimie tena, Lakini ikiwa itatokea, tunawaomba wahusika wasitunyime haki na uhuru wetu kuona.

Siyo kwamba kuzimia kwa Kikwete ni sinema nzuri sana, lakini kama tunavyolazimika kumuona akiongea, pia ni haki yetu kuona wakati chochote kinapotokea hasa akiwa katika maongezi. Sembuse kuanguka kwake kungetokana na risasi? Je serikali isingetaka kuziona tepu za camera zote kujua risasi ilivyatuliwa na nani na akiwa wapi? mbona kuzimia, camera zote ziamrishwe kubadili mwelekeo? Hiyo ni aibu ambayo serikali lazima ikubali kujirekebisha katika hilo. Ila kama kweli ni mgonjwa na akubali hivyo, basi Tanzania itakuwa ya kwanza kuongozwa na rais mwenye virusi na aliyekiri hadhani kuwa navyo. Kwa upande mwingine itawasaidia wagonjwa wa ukimwi kuishi maisha ya kawaida wakijua kwamba hata rais wao anao. Katika Afrika watu wanaougua Ukimwi hufa mapema kutokana na vidole wanavyonyooshewa. Wakijua ulikuwa rafiki wa kimapenzi wa FULANI na iwe huyo FULANI alikufa katika mazingara yaliyoashiria kuwa ni UKIMWI, basi vidole vyote vitaelekezwa kwako kwamba wanasubiri zamu yako ya kuondoka. Lakini Bwana Kikwete anaweza akabadili hali hiyo Tanzania. Akikubali kuwa MHADHIRIKA, basi wagonjwa wa UKIMWI watajua kwamba kuugua ugonjwa huo sio hukumu ya kifo. Mpira sasa uko kwa Kikwete

Vyombo vya habari kwenye mkutano wa CCM jipya lingekuwa gani? CCM ilileta uhuru Tanzania? Huo ni Wimbo tuliouzoea kwa zaidi ya miaka arobaini. Eti CCM ndio wanaoishikilia amani Tanzania? Lakini siyo baada ya mauaji ya kisiasa Zanzibar. Sasa jipya lilikuwa gani? Au ni nguo za kijani na njano? Hizo tumeziona tangu wadogo na hakuna maendeleo. Pengine kumuona Mkapa akimpigia debe Kikwete? Hiyo inaeleweka ili asisumbuliwe baada ya kuachia madaraka. Tangu Nyerere kumekuwepo utamaduni wa kulindana. Nyerere alimteua Mwinyi amfichie Madhambi jambo ambalo Mwinyi alionekana kulikataa. Ndio maana Mwinyi sio kipenzi cha wengi ndani ya CCM. Lakini kwa wananchi wanamwita Mzee RUKSA na anaheshimika sana kuliko Mkapa muuaji wa Waislamu Zanzibar. Lakini watakaomsumbua Mkapa siyo Kikwete, bali ni wananchi wa Tanzania ambao Mkapa aliwaibia alipokuwa madarakani. Tena kuna wale waliopoteza ndugu zao Zanzibar ambao hawatamwacha Mkapa alale usingizi. MKapa atajidanganya kwamba wakimtawaza Kikwete basi watanzania watayasahau madhambi yake. Hata kama hawatamfanya chochote, kilio chao kwa Mungu kinatosha kuwafanya viongozi wa CCM wazimie mikutanoni.

Jambo la busara kwa CCM ni kukubali kuachia madaraka kwa wengine. Kadiri wanavyozidi kubaki madarakani ndivyo wanavyoharibu zaidi. Tuseme CCM watumie mbinu zao chafu warudi madarakani. Halafu iweje? Watasema wamemshinda nani? Pesa ambazo CCM wanatumia kuhonga ili mradi wabaki madarakani, zinatosha kutengeneza barabara ya kutoka Arusha hadi Mwanza. Ni aibu kuwaona wakazi wa Mwanza wakilazimika kupitia nchi jirani ya Kenya ndipo waweze kufika Mwanza. Yaani Tanzania kuna amani nyingi kiasi cha barabara kutopitika. Imekuwa ni mtindo sasa kwa mabasi ya Tanzania yaendayo Mwanza kutoka Dar, kulazimika kupitia Nairobi kisha Nakuru, halafu Kericho na Kisii na mwisho yatokee Sirari Mpakani na kuingia Tarime Tanzania ndipo yafike Mwanza. Pamoja na kwamba watakuwa wamezunguka Kenya yote, safari hiyo ni fupi kuliko kutumia barabara ya Arusha Mwanza ambayo ni mbaya na isiyopitika. Hata hiyo Bwana Kikwete na Mkapa watatuambia ni Amani iliyoletwa na chama tawala CCM. Kodi alizokusanya Mkapa amejilimbikizia pesa kwa ajili yake na marafiki zake, na sasa anamtuma Kikwete akafanye hivyo hivyo. Hawana haya.

Wameumaliza upinzani Tanzania kwa hiyo hawana wa kushindana naye. Mbiyo zinanoga wakati wakimbiaji wanapokuwa wengi na wote miguu yao ni sawa tayari kwa mbio. Hapo ukishinda unastahili pongezi. Hata mpira haupendezi wakati upande mmoja unapoamua kuwavunja miguu wapinzani wao. Utacheza na watu ambao hawana miguu na kisha uwafunge magoli utegemee kushangiliwa? Hapana. Kinyume chake utazomewa. CCM wakijifanya kushinda uchaguzi kwa asilimia zozote hawatashangiliwa bali watazomewa. Dunia nzima itawashangaa wazee wazima wanaowakata miguu vijana kama kina Munishi, ili wabaki madarakani wakifanya hakuna. Vyombo vya habari vitaripoti nini? Itakuwa ni Hakuna jipya, Hatutarajii jipya, bali uoza ni ule ule wa miaka nenda miaka rudi. Sasa Kikwete ataleta nini kipya kama siyo kuongeza uvumi mitaani kwamba Rais wetu wa sasa ni MHADHIRIKA?
Kikwete siyo Wetu

Wakati Waislamu wameanza kumshuku Kikwete, Wakristo nao wanasema kikwete siyo wao. Magazeti yenye misimamo mikali ya Kiislamu yamemtaka Jakaya Mrisho Kikwete atangaze msimamo. Ama aachane na Uislamu abatizwe awe Mkristo, au abaki Mwislamu. Walihoji kwamba kikwete hawezi kuwa na dini zote mbili. Yaani hawezi kuwa Mwislamu Mkristo. Nao Wakristo kwa upande ule mwingine wanashindwa kabisa kumwamini Kikwete kwani wanajua wazi kwamba yeye ni Mwislamu.

Kwa Lugha inayoeleweka, Waislamu wanapomuona Kikwete na maaskofu, wanahisi kwamba huko amepewa nyama ya nguruwe awaletee msikitini. Nao Wakristo wanapomuona Kikwete kanisani kabla ya kubatizwa na kuukana Uislamu, Wanaona kama ametumwa na wenzao walete majini kanisani. Tayari Bwana Kikwete ana kibarua kigumu kuhusu imani yake kwa Mungu. Urais anautaka na Uislamu bado anaupenda. Ujanja wa wanasiasa kuwatapeli watu wa dini unafikia mwisho. Nyerere alifanikiwa kuwadanganya Watanzania kwamba CCM na serikali yake havina dini, Lakini baada ya Mkapa Mkristo kuwaua Waislamu Zanzibar, Watanzania wamejua kumbe serikali na CCM zina dini. Wanapotafuta mpaka wa dini na siasa wanakosa. Kwani wenye dini ndio wapiga kura. Tena kwa CCM kumteua Kikwete Mwislamu baada ya Mkapa Mkristo aliyekuja baada ya Mwinyi Mwislamu, Aliyechaguliwa na Nyerere Mkristo, sasa ni wazi kwamba dini mbili ndizo zinazopokezana uongozi Tanzania. Waumini wa dini nyingine wanaona wananyimwa haki na dini mbili ambazo zimeitawala Tanzania tangu tupate kile walichokiita UHURU. Kwa wale wasio na dini pamoja dini nyingine ambazo siyo Wakristo wala Waislamu, wakati sasa umefika nao wapewe nafasi ya kuiongoza Tanzania. Imegunduliwa kwamba Lugha ya Serikali haina dini ilitumiwa kuwapumbaza Watanzania kumbe kinachotawala ni DINI. Mbona baada ya Nyerere Mkristo alifuata Mwinyi Mwiislamu? Tena mbona baada ya Mwinyi Mwiislamu alifuatiwa na Mkapa Mkristo? Au tuseme yote ni bahati mbaya kwamba baada ya Mkapa, CCM wameona vyema wamteue Mwislamu Kikwete? Kama tutalazimishiwa Kikwete basi duara la Waislamu na Wakristo kuitawala Tanzania sijui litaishia wapi.Tunashangazwa na ukimya wa dini zilizoachwa nje ya uongozi huku wakidanganywa kwamba "Serikali haina DINI. Suluhu ni KATIBA iwaruhusu wagombea binafsi ili kila dini iteue mgombea wake. Magazeti ya kiislamu yana haki ya kujua kama kweli Kikwete wa CCM ni Mwislamu mwenzao. Badala ya magazeti ya Kikristo kuhoji kama Kikwete atalipiza kisasi cha Mkapa kuwaua Waislamu, wao wanapayuka hovyo. Mfano ni gazeti la "Habari Njema" Linalokosoa gazeti la kiislamu.



Kikwete ni wa CCM

Kikwete wa Jakaya ni uteuzi wa CCM. Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Kwamba CCM wamemteua mtu wao, hiyo siyo sababu tosha kulifanya Gazeti la Kikristo kuanza kupayuka. Mbona? Habari Njema wanasahau kwamba wanasiasa ni WAONGO. Sasa wanalitapeli Kanisa. Badala ya Gazeti la kidini kuwaonya kondoo dhidi ya MBWA MWITU wanasiasa, Wao wanaanza kufurahia posho wanayotupiwa kama KUKU atupiwavyo mahindi kumbe yanaashiria mwisho wake. GTV Tumekataa kumeza ndoano ya CCM hata waweke chambo gani. Tutatumia kila lililo ndani ya uwezo wetu kuwaonya Watanzania wajihadhari na mnyama huyu CCM. Amewameza wenzetu kwa zaidi ya miaka arobaini, na sasa anatutapeli tumwachie nafasi aendelee kutumeza kwa miaka mitano ijayo. Haiwezekani, Hatukubali, Hatutaki, Tena tumekataa.

Uhuru wa CCM kumteua Kikwete wa Jakaya, unapaswa kuishia pale uhuru wetu kuteuliwa kama wagombea binafsi unapoanzia. Kuanza kushangilia na kutumia pesa za walipa kodi kununua nafasi kwenye vyombo vya habari ili kutoa kauli za kiburi, Hakutaisaidia CCM. Ikiwa gazeti la kiislamu liliandika kwamba Waislamu hawamtaki Kikwete kwani ni kibaraka wa KANISA, "Habari Njema" Wangepaswa kumkemea Kikwete aache kulitumia Kanisa kwa manufaa yake kisiasa. Akifikiri anajitengenezea mazingara ya kukubaliwa na Wakristo, atajikuta pabaya. Waislamu wameanza tayari kumkana kwamba yeye kikwete si mwenzao. Wakristo nao sidhani kwamba watadanganyika na tabia ya ghafla ya Kikwete kuwa mgeni makanisani. Wengi wameanza kuifananisha tabia hiyo na pipi apewazo mtoto aache kulia. Wanasiasa Tanzania bado wanafikiri kwamba Watanzania ni watu wasioweza kuchambua mambo. Mwislamu Kikwete anapoanza kuingia kwenye majumba ya ibada {MAKANISA} bila kuukana uislamu ni sawa na kuwatania wenye imani hizo. Kifupi niseme "ANAKUFURU." Sambamba na hilo, Mkristo Benjamin Mkapa anapojifanya kuingia misikitini bila kusilimu awe Mwislamu, hiyo ni KUFURU kwa dini ya Kiislamu. Nasema hivyo kwa sababu wote wanajua nini kinapaswa kufanyika ndipo mtu awe muumini wa dini. Kuyakataa masharti ya dini husika na uingie humo ukiwa KAFIRI, kisha utoke humo ukiwa umewadanganya, hiyo inaonyesha kukosa adabu kwa Mungu anayeabudiwa na watu hao. Ikiwa wanasiasa hawawezi kuikosea adabu bendera ya nchi, Vipi wakose adabu kwenye sehemu za kuabudia??? Wanakuja makanisani na ahadi za uongo. Wachungaji na Mashehe wanakubali vipi wanasiasa waingize unajisi Makanisani na Misikitini? Sehemu Takatifu mnakubalije Kikwete aingie na uchafu wake na atoke akiwa amewachafua? Kulingana na imani ya Kikristo Kikwete Mwislamu lazima aukane uislamu ndipo apewe nafasi ya kufanya chochote Kanisani. Mambo ni hivyo hivyo Misikitini. Kafiri hawezi kuruhusiwa kuingia Msikitini akiwa amevalia viatu, huku amebeba nyama ya nguruwe. Hiyo ni KUFURU na kuikosea adabu KORAN TUKUFU. Wanasiasa wanapoingia Misikitini kwa lengo la kuwadanganya Waislamu wawaunge mkono, ni sawa na kuingia na nguruwe msikitini. Wanakuja na pesa za Rushwa na wanawanunua wakuu wa dini. Hilo ni kosa linalopaswa kukemewa na magazeti yote ya kidini. Tunalishangaa "Habari Njema" Gazeti la Kikristo kuanza kumpigia Debe Kikwete wa Jakaya na kusema ni wa wote. Wangefanya vizuri kusahihisha hilo na kusema Kikwete ni wa Jakaya na tena wa CCM. Watanzania wana mtu wao.Tunachoomba ni kwamba Watanzania wapewe nafasi ya kumchagua yule watakaeona anawafaa kuwaongoza. Kujaribu kuwalazimishia Kikwete, msishangae akiwa kiwete kama Mkapa. Nyerere alitulazimishia Mkapa, akatoka akiwa kiwete, Mkapa asijaribu kutulazimishia Kikwete kwani Mungu anajua nini cha kufanya na wale wanaowatesa Watanzania. Sina tatizo na uteuzi wa CCM, lakini namuomba Bwana Kikwete asije Kanisani kwangu kututapeli kwamba yeye anatupenda Wakristo. Ikiwa anaupenda kweli Ukristo, Kipimo chake ni aikubali Injili ya Yesu, Kisha amwamini Yesu badala ya Mtume Mohamad, Halafu tumbatize aitwe jina lolote hata kama akipenda kubaki na jina lake Kikwete hatuna tatizo hapo. Akikubali hayo tunamkaribisha kanisani. Lakini siyo aje kutuletea pesa za wizi.Huku akijifanya anachangia miradi ya dini ya Kikristo. Gospel TV tunaunga mkono gazeti lililomkosoa Kikwete na kusema kwamba Waislamu wamemshitukia Kikwete. Nasi GTV tunasema kwamba hata Wakristo wa kweli, Tumemshitukia Kikwete. Labda ajaribu mbinu nyingine. Lakini hii ya kuja Kanisani mwenye dhambi halafu aondoke ametuingiza dhambini tumeikataa sawa na tulivyomkataa shetani na mambo yake yote.

Wanasiasa Huaribu taratibu za ibada

Aliyekuwa Rais wa mabavu na Jazba Tanazania Mzee Mkapa akiwatapeli Maaskofu kwamba serikali haina dini.

Kuwakubali wanasiasa wasiyoiamini Injili makanisani, ni sawa na kumwalika Shetani Kanisani. Fikiri usumbufu Waumini wanaoupata wakati mtu kama Kikwete anapolitembelea Kanisa. Kwanza askari kanzu wanalitembelea kanisa siku tatu kabla ya ziara. Kanisa linapekuliwa kila kona. Wanaofanya kazi hiyo ni askari walevi wasio na sare za kazi. Eti wanahakikisha kwamba Kikwete atakuwa salama Kanisani hapo. Siku ya ziara ikifika, Kanisa linavamiwa na askari wenye silaha kali. Nusu ya watu watakaolijaza kanisa siku hiyo ni maofisa usalama wa Taifa, Pamoja na maofisa usalama wa Kikwete. Watakuwa wamevalia kiraia, lakini nyuso zao zitakwambia hawa siyo waumini wa kawaida. Hata ibada itawashinda kufuata kwani hawajui chochote kuhusu Kanisa. Mchungaji wa Kanisa ambaye alipaswa kuandaa mahubiri kwa waumini, analazimika kuandaa ujumbe uliojaa sifa kwa Kikwete badala ya Mungu. Usisahau kwamba mchungaji huyo alilazimika kusimama nje kwa masaa zaidi ya mawili akimngoja mgeni rasmi Kikwete aingie Kanisani hapo. Huu ndio usumbufu tunaoufananisha na kumwabudu mwanadamu badala ya Mungu. Ibada ya siku hiyo inageuka kutoka kumwabudu Mungu, na inakuwa ibada ya kumwabudu kikwete. Ndio maana tunapinga tabia ya wanasiasa kutumia sehemu za ibada kuabudiwa badala ya Mungu. Hatupingi mtu yeyote kuingia kanisani au msikitini, lakini mtu huyo hata akiwa nani, anatakiwa afuate utaratibu wa dini husika. Kutatanisha ibada za watu eti ni Kikwete anakuja, Hiyo ni tabia wakuu wa dini wanapaswa kuipinga kwa nguvu zote. Kikwete hawezi kuchukua nafasi ya Mungu. Akija Kanisani aje kama muumini mwingine yeyote. Mambo ya kuingia kanisani na kikosi kizima cha kumlinda huku wakiwa na silaha kali, pamoja na macho ya kuwatisha waumini yanatakiwa yakomeshwe mara moja. Kwa nini Kikwete awasumbue waumini kwa vishindo vya kuingia Kanisani na kuichukua nafasi ya Mungu? Viongozi wa dini wangejua ibada inavurugwa kiasi gani anapoingia mtu kama kikwete, wangemsihi akome kuingia humo na mbwembwe za kuwatisha waumini.Wanasiasa ni watu wanaopenda kutisha. Mahali pa kutembea kwa miguu wao watatumia gari zaidi ya kumi. Askari wa usalama barabarani watatangulia na pikipiki zaidi ya tano, halafu zitafuatiwa na Land Rover mbili zilizojaa wana FFU na bunduki pande zote, Halafu yafuate magari zaidi ya kumi na bado la Bwana Kikwete halijawasili. Mchungaji atalazimika kusimama kwa muda mrefu akisubiri Kikwete aingie. Akiingia, Utaratibu wa Ibada unavurugika na wa Kikwete unaanza. Usumbufu huu ndio tunaosema kwamba hatuutaki. Wanasiasa wafanyie kampeni zao nje ya majumba ya ibada.

Kikwete na Kanisa Kwa muda gani?

Tunajua wazi kwamba Kikwete na kanisa sasa watakuwa kama pete na kidole. Lakini kwa muda gani? Wanasiasa huwaadaa watu wa dini wanapotafuta kura. Lugha kama Kikwete ni wa wote hazitaisha midomoni wakati wa uchaguzi. Unafiki huu tunataka ukome. Uongozi siyo kuikana dini. Inawezekana mtu akawa kiongozi bila kuikana dini yake. Ukija kanisani kwa kuwa unataka kuchaguliwa, huo ni UNAFIKI. Kama kweli ulikuwa mtu wa dini zote, basi tungekuona kanisani tangu mwanzo na siyo wakati wa uchaguzi. Hivi wanasiasa wanamdanganya nani? Mungu au wanadamu? Watu wa dini wakiwakosoa wanasiasa wanaowaua watu bila sababu, wanaambiwa wasichanganye dini na siasa. Kwa maneno mengine, Mkapa Mkristo ana uhuru wa kuwaua waislamu Zanzibar, na asiulizwe chochote na waislamu wala Wakristo. Eti wakiuliza, wanachanganya dini na siasa. Mgombea urais akiwa Mkristo, Ataanza kuwatapeli waislamu kwa kujifanya anachangia miradi ya maendeleo misikitini. Akishachaguliwa mambo yanakuwa kinyume. Mfano mzuri ni Mkapa. Alipokuwa akiomba kura, alisema yeye ni Rais wa wote. Alipochaguliwa alianza kuwabagua Waislamu. Aliungana na Amerika kuamini kwamba kila Mwislamu ni Ghaidi. Ikawa kupata hati ya kusafiria ukiwa Mwislamu ni sawa na ndoto. Hayo yote yanafanyika chini chini, huku Mkapa akihubiri kwamba yeye ni Rais wa waislamu na Wakristo. Huu ni unafiki tunaotaka ufike kikomo. Ikafika siku ya siku. Ndugu zetu Zanzibar wakatumia haki yao ya kikatiba kusema kwamba hawaitaki CCM. Mkapa Rais Mkristo, akaamuru Waislamu zaidi ya sabini wauawe, na wengine wakakatwa viungo vyao ili kuwafundisha adabu. Wakristo wenye mtazamo kama wa gazeti la Habari Njema wakashangilia. Walichosahau ni kwamba wanasiasa katika kulinda maslahi yao wanaweza kuua yeyote. Munishi Mkristo niliposema kwamba si haki Mkapa kuwaua Waislamu, Kanda zangu zilipigwa marufuku Tanzania, Mkapa Huyo huyo Mkristo, akaamuru nikamatwe, na Polisi Tanzania wakatangaza kwamba wananisaka. Rais Mkristo anamtafuta Mchungaji Mkristo amuue kwani Mchungaji alimkemea alipowaua Waislamu. Hiyo ndiyo siasa. CCM na huyo waliyemteua wawadanganye wengine lakini GTV Hatudanganyiki na unafiki wao.Kinachotushangaza zaidi ni kwamba wakati wa KAMPENI ni bado. Tena uchaguzi ni bado. Isitoshe vyama vingine havijatangaza wagombea wao. Gazeti la dini limeanza KUPAYUKA. Serikali nayo inafurahishwa na habari hizo. Ikiwa kanda za Munishi zilifungiwa kwa kusema Mkapa ni MUUAJI, Vipi gazeti la Habari njema halijafungiwa kwa kusema kwamba Kikwete ni wa watu wote? Si hapo pia wamechanganya siasa na dini? Ikiwa mnapokea SIFA, Mbona maonyo mnayafungia nje? Ni unafiki huu ndio ulionifikisha mahali pa kusema, "Siasa ni uongo, na kwamba wakati umefika kwa watu wa dini zote kujitenga na siasa. Kila dini ianze harakati za kujikomboa kutoka minyororo ya wanasiasa. Tutafanikiwa hilo kwa kuishinikiza serikali ya CCM kuibadili KATIBA ili iwaruhusu wagombea BINAFSI. Katiba ya sasa inasema mtu hawezi kuwa Rais bila kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa. Nasi tunasema, Huwezi kujiunga na uongo ili uwatoe waongo.Kwani siasa ni uongo.

Uvumi Mitaani

Kuna uvumi kwamba Kikwete wa CCM anapenda sana kwenda DISCO usiku. CCM hawakukosea waliposema Jakaya Kikwete ni kijana. Miaka 55 na kufanya mazoezi pamoja na kula vizuri, kumemfanya Kikwete audanganye umri wake. Kweli anaonekana kijana jambo linalompatia marafiki wengi wa kike na wa kiume. Sura yake ikilinganishwa na Mkapa, Kikwete anaweza samehewa mengi kwa kuangaliwa usoni tu. Wakati Mkapa akiongea tu watoto wanaingia uvunguni kwa kuiogopa sura tu. Duru kutoka wanaomfahamu Kikwete kwa karibu, Wanasema huyo Bwana siyo mchezo. Wanasema ukikutana naye akiwa amevalia JEANS na fulana nyepesi jioni, Labda mtu fulani akushitue huyu ni Mheshimiwa Kikwete. Lakini hivi hivi tu, huwezi kumtambua. Wanasema Jakaya Kikwete alichangia sana katika kusababisha Mwanamuziki mmoja nchini Tanzania kufungwa jela maisha pamoja na Familia yake yote.. Inadaiwa mwanamuziki huyo alimbusu mmoja wa marafiki wa kike wa Kikwete. Duru hizo zilitufahamisha kwamba Kikwete akitumia ushawishi mkubwa alio nao Serikalini aliwaamuru Polisi wamsukie kesi nzito mwanamuziki huyo. Kweli mwanamuziki huyo alikamatwa pamoja na jamii yake yote na kufunguliwa shtaka la kuwabaka watoto zaidi ya kumi Akiwa yeye na jamii yake. Hukumu ya kesi hiyo ilikuwa kifungo cha MAISHA kwa familia yote. Hiyo ni hukumu ya kwanza duniani. Kwenye ulimwengu wa Siasa na Wanasiasa chochote chaweza kutokea. Ama kweli CCM safari hii, wametuletea kijana kweli. Ikiwa Kikwete waziri anaweza sababisha Familia nzima kwenda jela maisha. Akiwa Rais Mungu apishe mbali asije akaamuru mkoa mzima uchomwe moto. GTV tunasema kama ni kweli Mwanamuziki huyo alifungwa kwa sababu za kisiasa, Tunaitaka Serikali imwachie huru mara moja bila masharti yeyote.

"Kikwete Tosha" asema Mchungaji

Mchungaji Paul M.K. Mduma aliyekuwa Mkurugenzi wa Muziki kwaya ya Uinjilisti Arusha mjini kabla ya kuhamia Kenya na kutawazwa kuwa Mchungaji wa kanisa la AIC (Afirican Inland Church) Ameishi Kenya kwa miaka 10 na Kwa sasa hivi yuko Arusha Mjini kama Mhubiri wa kujitegemea akifanya kazi na makanisa yote yanayomwalika, huku bado akiwa msharika wa KKKT Usharika wa Arusha Mjini.

Kufuatia malumbano kati ya magazeti ya Kiislamu na Kikristo kumhusu Kikwete, Mchungaji Paul Mduma amejitokeza kusema "Kikwete Tosha." Akiwa katika Ofisi za GTV Nairobi Kenya mchungaji Mduma alielezea masikitiko yake kwamba, vyombo vya habari vimeanza kumchafua Kikwete aliyemjua tangu akiwa mwanafunzi Kibaha Secondary School. Alidai kwamba walisoma wote kwa muda wa miaka minne. Tangu mwaka 1966 hadi 1969 wakati Kikwete alipochaguliwa kwenda Tanga High School kidato cha tano na sita. Mchungaji mduma aliongeza kusema: "Japo sikuchaguliwa kuendelea na masomo ya juu kama Kikwete, Sina chuki binafsi naye na nitamsifu inapostahili. Kwa hiyo kuhusu masuala ya kumjua Kikwete hakuna wa kufananishwa nami Mchungaji mduma." Alisisitiza mchungaji.

Akizungumzia uhusiano wa Kikwete na wanafunzi wenzake Mduma alisema: " Kikwete alikuwa mpigania haki shuleni jambo lililopelekea kuchaguliwa kuwa Rais wa shule (School President) Aliitumia nafasi hiyo vyema na alitokea kupendwa sana na wanafunzi na hata waalimu, Hususan Mwalimu wa michezo Mr. Konic Pamoja na Head Master wetu Paul Figveg. Siyo kwamba Kikwete alikuwa maarufu kwa masomo pekee, bali alikuwa mpenda michezo hasa mchezo wa mpira pamoja na kupokezana vijiti. Shuleni wanafunzi walikuwa wakimwita "OJUE" Jina lake maarufu la michezo.

Ni sababu hizo na nyingine ndizo zinazomfanya Mchungaji Mduma aseme Kikwete Tosha. Anadai kwamba Watanzania watakosea sana kumchagua mtu mwingine isipokuwa Kikwete, Tena anausifu umaarufu wa Kikwete kutatua matatizo jambo alilosema liliwafanya wakuu wa Chuo Kikuu kumwita atatue mizozo ya wanafunzi wakati Kikwete alikuwa Sekondari. Mduma anadai kwamba uwezo huo wa Kikwete atautumia kutatua matatizo mengi duniani kama watanzania watampa kura.

Kauli ya Mchungaji Mduma itapokelewa kwa hisia tofauti hasa tukizingatia kwamba Waislamu wanamuona Kikwete kama Kibaraka wa Kanisa, Huku Wakristo wakishindwa kumwamini kwani wanadai Kikwete ni Mwislamu anayeweza kutumia nafasi yake kama Rais kuisilimu Tanzania. Mchungaji Mduma alisema hiyo siyo sababu. Kikwete alienda kuchangia Kanisa na siyo kuendesha ibada za Kanisa. Kanisa ni chombo cha jamii kwa hiyo siyo kosa kwa kiongozi kuchangia miradi ya kijamii bila kujali dini yake. Aliongeza kusema kwamba Kwa Kikwete kuyachangia Makanisa ni kama kurudisha shukrani kwani yeye Kikwete alisomea shule za misheni. Lakini mbona kurudisha shukrani huku kumekuja wakati wa uchaguzi? wengi wanajiuliza kwa nini Kikwete asingefanya hivyo wakati akiwa waziri?

GTV Tulipomuuliza Mchungaji Mduma nini maoni yake kuhusu wachungaji wanaomsakama Kikwete kwa sababu za udini? Yeye aliwaita wachungaji kama hao WANAFIKI. Alihoji kwamba wakati wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Maaskofu walikuwa wakimwalika katika sherehe za kuwasimika Maaskofu kwenye kazi ya Mungu. Hawakuita waziri Mkristo bali walimwita Rais wa wakati huo Mwinyi. Iweje sasa ubaya ambao hawakuuona kwa Mwinyi wauone kwa Kikwete? Aliwataka kuachana na mawazo potovu ya UDINI ambayo yanaweza kuitumbukiza Tanzania katika matata yasiyo na sababu. Alimaliza kwa kusema kwamba Tanzania ni nchi ya amani na hawezi kukubali watu wachache kutumia dini kuvuruga amani.

Pastor Mduma ana haki kutoa maoni yake. Lakini....
.
Mchungaji Kikwete akihubiri? Hapana. Huyu ni Kikwete Mwislamu, Tena mwanasiasa akiwatapeli Wakristo Kanisani tena madhabahuni.

Kwenye maoni yake Mchungaji Mduma alihoji kwamba Kikwete hakwenda kanisani kuhubiri, kwa hiyo madhabahu ilikuwa mbali naye. Lakini kwenye picha hii tunaona Kikwete akiwa amekabithiwa Madhabahu ya Bwana, huku wachungaji na Wakristo wakisubiri kupewa meza ya Bwana na Mwislamu Kikwete. Ni KUFURU hii katika nyumba ya Bwana ndiyo inayotufanya tushindwe kuunyamazia udhalimu huu Kanisani.Yesu akishuka leo akute nyumba ya Baba yake imegeuzwa kuwa pango la wanyangayi na wezi kama kina Kikwete, Hatuna shaka kwamba atazipindua meza na kuwachapa bakora wachungaji waliomruhusu Kikwete kuingiza unajisi katika nyumba ya Bwana. Pia hatudhani kwamba Kikwete ataepuka bakora za Yesu kwa kutumia pesa CCM walizowaibia Watanzania kuyanunua Makanisa. CCM wakitumia pesa walizoiba, wameweza kununua kila kinachowezanunuliwa, Lakini kujaribu kumnunua Mungu kunaashiria mwanzo wa mwisho wao. Wamecheza na kila mtu, lakini kumchezea Mungu kutawapeleka pabaya. Wanadanganyika na nguvu ya pesa ambazo hazikuweza kumponya Nyerere wakati Mungu aliposema kuwatesa Watanzania sasa basi. CCM walitumia pesa kwa marundo kujaribu kumponya "mungu wao Nyerere, lakini jitihadi zao ziligonga mwamba pale Nyerere alipoiaga dunia.Wengi wakati huo tulifikiri kwamba CCM wamejifunza na wangeyarekebisha makosa yao. Kinyume chake Mkapa aliongeza kidonda juu ya kidonda pale alipowaamuru polisi wawaue waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar. Kwa kuwa Mungu siyo Athumani, Mkapa alichapwa kiboko na mifupa ikaanza kusagana yenyewe. Kama kawaida yao, CCM wakatumia "Burungutu" la pesa kujaribu kumponya Mkapa. Hata sasa tunapozungumza, Mkapa hali yake kiafya ni mbaya. Kwamba anaishi kwa nguvu za dawa, haina maana amepona. Machoni pa Mungu Mkapa ni suala lililokwisha malizika. Kwamba tunamuona akitembelea magongo, hiyo ni ishara kwamba pesa zinaweza kusitisha mwisho, lakini siyo mwanzo wa mwisho wa Mkapa. Tayari mwanzo wa mwisho wake umeanza. Ngojeni amalize kipindi chake cha urais, halafu tume ya uchunguzi iundwe kuchunguza alivyotumia madaraka, kisha apelekwe mahakamani kujibu mashitaka ya kuwaua waaislamu zaidi ya 70 Zanzibar, muone kama atakuwepo kuisubiri kesi imalizike. Hukumu ya Mkapa tayari.Utekelezaji wake umeanza.Ajabu ni kwamba CCM hawalioni hilo.Bado wanajigamba kwamba wao ni nambari one. Kile ambacho CCM hawakioni ni kwamba Mungu ameanza kuwashughulikia. Mmoja baada ya mwingine watatoweka baada ya kuchapwa bakora na Mungu mwenyewe.Watanzania hawana uwezo wa kipesa kupambana na CCM, Lakini Mungu hawezi kuwaacha wamalizwe na mnyama huyu CCM. Mungu anasema sasa basi. Imetosha. Watu wangu wameteseka kwenye mikono ya CCM vya kutosha.Ikiwa CCM hawataachia madaraka kwa Watanzania, Basi Mungu atawamaliza mmoja baada ya mwingine.Kila mtu ataugua, lakini anapougua yule anayewaua Watanzania bila sababu, Hatuwezi kumuomba Mungu amponye ili aendelee kutuangamiza. Sambamba na hilo hatuwezi kuingilia kazi ya Mungu na kuutoa uhai wake.Lakini Mungu mwenyewe akianza kuwashughulikia CCM na waanze kuonyesha dalili za kutoweka katika uso wa dunia, hatuwezi kushangilia, wala hatuwezi kumuomba Mungu awaponye. Yetu ni macho na masikio, na kusema Mapenzi ya Mungu yatendeke.

Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais Tanzania Mzee Kawawa akielekezwa kwenye Wadi kulazwa. Inasemekana anasumbuliwa na mifupa. Yeye na Nyerere ndio waasisi wa siasa ya Ujamaa Tanzania. Inasemekana Kawawa katika kuitekeleza siasa ya Ujamaa, alisababisha vifo vya mamia ya Watanzania pale alipowahamisha makwao na kuwapeleka msituni ambapo vijiji vya Ujamaa vilitarajiwa kujengwa.Watanzania wengi wakati huo walipoteza maisha yao kwa kuliwa na wanyama pori. Na wengi walikufa kwa njaa pamoja na magonjwa yaliyosababishwa na kurundikwa mahali pamoja msituni bila maji wala matibabu.

Wanaomjua Kawawa wanasema yeye alikuwa Mjamaa kuliko Nyerere mwanzilishi wa Ujamaa.Katika kuitekeleza siasa ya Ujamaa, Kawawa ndiye aliyefanya makosa mengi kuliko wote.Lakini kwa sababu Nyerere ndiye mwanzilishi wa siasa hiyo mbovu, lawama nyingi anatupiwa yeye kwani Kawawa na wengine walikuwa watekelezaji tu.CCM haijawaomba Watanzania msamaha kwa kosa la kuanzisha siasa ya ujamaa ambayo iliwafanya Watanzania wengi kupoteza maisha yao.Miaka zaidi ya arobaini madarakani, CCM hawajatosheka na kumwaga damu za Watanzania. Bila aibu wla kuona haya usoni, CCM wanawatapeli Watanzania wawachague kwa kipindi kingine cha miaka mitano.Hawana Adabu.Wauaji wakubwa.Wezi wa mali za Umma. Chama Cha Majambazi kinawaomba Watanzania nafasi nyingine ya kufanya ujambazi. Punguani ndiye atakayewapa kura yake. Lakini mwenye akili timamu, boro aitupe kura hiyo chooni kama amekosa wa kuchagua kuliko kichagua CCM.Kwamba wamemteua Kikwete haiwezi kuwatoa katika kundi la Majambazi. Wanasema Kikwete ni safi. Sawa. Lakini alikuwa anafanya nini na Majambazi CCM? Kikwete ni mbwa mwitu anayetujia akiwa na mavazi ya kondoo. Watanzania misidanganyike. CCM Haitufai. Ni mbaya. Imezeeka.Tusiirudishe madarakani tena.Siyo Kikwete hata nani akija na jina la CCM hatufaii.



Mchungaji Faustin Munishi Rais Mtarajiwa Tanzania Amesema kwamba Hakuna uchaguzi Tanzania bila ya Katiba mpya.
Watakaowaburuza Watanzania kuingia kwenye uchaguzi bila katiba kubadilishwa, wajue wanafanya hivyo kinyume na matakwa ya Watanzania walio wengi. Alisema: "
Nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania bado iko pale pale. Kwamba katiba hairuhusu wagombea binafsi, hiyo hainifanyi nijiunge na chama chochote cha kisiasa ili nitimize masharti ya KATIBA. Kwangu siasa ni uongo, na siwezi kujiunga na uongo niwatoe waongo. Ikiwa CCM hawataibadili Katiba iruhusu wagombea binafsi, basi tutaiasi katiba tuandike yetu. Wakichaguana nasi tutachaguana. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa KATIBA ya Injili na serikali ya Injili, Rais wa Injili na Bunge la kiinjili. Hapo ndipo tunapoelekea. Siyo ajabu kwani tayari tuna nyimbo za GOSPEL kilichokuwa kimebaki ni KATIBA ya Gospel Itakayounda tume ya Gospel ya uchaguzi utakaomchagua Rais wa Gospel atakayeunda Serikali ya Gospel akitumia wabunge wa Gospel. Waislamu wakiona vyema wajiunge na Gospel tutawakaribisha. Wakiona waunde yao ya SHARIA, ni sawa. Pia kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa nchi ya serikali zaidi ya kumi. nayote hayo yatafanyika kwa amani. Kikwazo cha amani Tanzania kitakuwa ni CCM pale watakapokataa mabadiliko, na kungangania madaraka.Kama kawaida yao wataanza kuwalaumu wengine. Lakini wananchi safari hii wameerevuka na wanamjua mbaya wao ni nani.CCM ndiye nyoka anayestahili kupondwa kichwa."

KATIBA SIYO MALI YA CCM

Katiba ya Tanzania ni ya watanzania. Siyo mali ya CCM. Lazima kila mtanzania ahusike katika kuirekebisha au kuibadili. Kuna mengi yanayohitaji marekebisho na mengine yatatolewa kabisa. Najua kwamba nikiingia ikulu na katiba ya sasa itanikwamisha mengi. Tanzania ni sawa na gari iliyonoki injini. Inataka  matengenezo kamili ndani ya injini. Siwezi kuifanyia Tanzania MAREKEBISHO INAYOSTAHILI bila ya katiba mpya. Hata kama kipengele kimoja kitabadilishwa niweze kugombea bila chama cha kisiasa, hilo siyo lengo langu.

Lengo langu ni kuleta mabadiliko ambayo ndiyo kiu ya watanzania wengi wakubwa kwa wadogo. Hatuwezi kuwa na nchi yetu, bila katiba yetu. Tena katiba haiwezi kuwa yetu kama haina mchango wa mawazo yetu. Tunahimiza zoezi la kukusanya mawazo kutoka kwa watanzania wote lianze ndipo katiba irekebishwe. Bila hilo kufanyika  hakuna sababu ya kufanya uchaguzi kwani CCM watatumia mapungufu yaliyoko kwenye katiba kushinda uchaguzi kiulaini.

Tumeliona hilo. Ndiyo maana tunasema kwamba hakuna aliyehitimu kuingia katika uchaguzi na katiba ya sasa. Ina mapungufu mengi, Hatuitaki, Ni batili. Yeyote atakaeingia kwenye uchaguzi na katiba ya sasa ajue anafanya hivyo kinyume cha sheria. Ndiyo ni kinyume cha sheria kwa sababu Watanzania wengi wanataka KATIBA MPYA. Kujaribu kuwaburuza ili waingie kwenye uchaguzi bila ya kuibadili katiba ni mbaya kuliko wao kuchukua silaha na kuanza kudai haki zao kwa mtutu wa bunduki. Hatuombi hali ifikie hapo kwani itatuumiza wote. Lakini ikibidi, Hakuna jinsi.


Kuhusu baraza la mawaziri, nilisema wazi kwamba mimi sitakuwa na uwezo wa kuunda baraza la mawaziri. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda baraza lake la mawaziri. Katiba mpya italiruhusu bunge kuunda baraza letu la mawaziri. Sifa za watakaogombea nafasi za uwaziri lazima ziambatane na taaluma zao katika wizara husika. Wakati wa kuchaguliwa waziri kwa sababu za kikabila, kiundugu na kirafiki, UMEKWISHA. Hata hapa kuna wengi tayari nimeona wataifaa Tanzania katika baraza la mawaziri. Mtu kama Augostino Moshi ukisoma posti zake utaona uanasheria ndani yake.


Hawa ndio tunaotaka kuwahimiza wagombee nafasi za waziri wa sheria na katiba. Wabunge wakiridhishwa na kuhitimu kwao katika fani husika watawachagua.
Nimemtaja Moshi siyo kwa sababu ni mchagga, bali nipate nafasi ya kujibu swali lake. Aliniuliza kama nakimudu kiingereza. Ukweli ni kwamba kiingereza nakimudu vizuri.

Lakini nilijifunza kwa njia ngumu zaidi. Nikija Nairobi mwaka 1984 nilikuwa siwezi kabisa kuwasiliana kwa kiingereza. Jambo hilo lilinikera sana. Niakaamua kuanzia mahali. Biblia ndicho kitabu kilichokuwa hakibanduki mikononi mwangu. Nilikuwa nimemaliza kuisoma na kuirudia mara tatu. Nikanunua madaftari makubwa ya kuandikia kama matano, halafu nikanunua Biblia ya kiingereza. Nilianza kuandika neno hadi neno, nikamaliza kuandika agano jipya. Mengi nilielewa maana kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimeyasoma katika Biblia ya kiswahili. Yaliyonishinda matamshi ilinibidi ninunue biblia katika kaseti. Yale ambayo sikuelewa kuyatamka, Biblia ya kaseti ilinisaidia kujua yanatamkwa vipi.

Hata kabla ya kumaliza agano la kale tayari nilikuwa na kiingereza kingi sana akilini mwangu. Tayari niliweza kuwasiliana kwa kiingereza kuliko.  Nasita kusema kuliko wasomi wengi Tanzania, lakini ukweli unabaki hivyo. Sasa hivi ndipo kasi ya kujifunza kiingereza imeongezeka Tanzania. Wakenya na Waganda wamefungua shule uchwara na wanaziita za kimataifa kwa sababu tu wanazingatia somo la kiingereza. Ningekuwa najua kutumia kompyuta wakati huo, nisingepitia njia ngumu hivyo kukijua kiingereza.

Lakini sijuti kwani maneno mazito ndani ya Bibilia yamekiongezea uzito kiingereza ninachotumia kuzungumza na hata kuandika. Sitaki nijisifu kwamba Kiingereza changu ni sawa na kile cha malkia wa UINGEREZA, lakini nitakuwa mpumbavu gani nishindwe kujieleza kwa lugha rahisi kuliko zote duniani? Kiingereza kwa sasa ndiyo lugha rahisi kuitumia kuliko hata kiswahili. Haya niliyoyaandika hapa hakuna mahali  katika kompyuta naweza kufanya "SPELL CHECKING", sababu ni kiswahili.  Lakini ingekuwa kiingereza, bila kujali natumia programu gani nitapata mahali pa kuisahihisha kazi yangu kiulaini.

Ni urahisi huo ndio unaonipa mashaka kwamba wengi hawajui kiingereza. Kuna rafiki yangu simtaji. Ni mwandishi wa habari katika gazeti la NATION lichapishwalo kwa kiingereza kila siku nchini Kenya. Ukisoma makala zake, utapenda. Mpangilio wa lugha, usahihi wa maneno, NK. Lakini wacha akuandikie barua ya mkono, Au akutumie ujumbe mfupi kwa simu za kipepesi. Utashangaa mbona kiingereza chake kibovu?

Kumbe amelemazwa na kompyuta ambayo inamfanyia kila kitu kuanzia "SPELL CHEKING" mpaka na mtiririko wa lugha. Je ni kitu cha kujivunia kujua kiingereza? Hapana. Hata wanaokiongea au kukiandika vibaya siyo makosa yao. Siyo lugha yao ya kwanza maishani.

Pamoja na umuhimu wa kiingereza duniani leo, Siungi mkono kasi watanzania waliyo nayo katika kukikimbilia kiingereza. Wengi wanalipa pesa za kutisha kwenye shule ambazo zinatilia mkazo kiingereza, Wengine wanawapeleka watoto wao nje Kenya Uganda, Na hapo nimetaja sehemu chache sana. Yote ni watoto wajue kiingereza. Kuna tofauti kati ya kuelimika na  kujua lugha. Lakini kwa watanzania wengi hilo hawalijui. Wanafikiri kuelimika ni kujua Lugha. Kuna uwezekano wa kuzijua lugha tofauti bila kuwa na elimu. Lakini kiingereza tu, sioni ulazima wa wazazi Tanzania kwenda kasi wanayokwenda kukifukuzia kiingereza. Kuna njia nyingi za kuweza kuijua lugha yeyote bila kuingia gharama kubwa wanazoingia watanzania.Nimalize kwa kusema kuna njia nyingi za kumuua panya. Ukiweka mtego utamnasa atakufa. Ukiweka dawa ya sumu jikoni, panya atakula na atakufa. Lakini ole wako mtoto wako akidhani hiyo uliyoweka jikoni ni peremende. Uliyotarajia yampate panya yatampata mtoto wako.

Watanzania wengi wameamua kumuua panya wa kiingereza wakitumia sumu jikoni. Tayari nimeiona hatari mbele yao. Nani awaambie njia nyingine rahisi ambayo ni kumchagua Munishi awe rais wa Tanzania chini ya katiba mpya nitainua kiwango cha elimu. Kiwango cha elimu kikiinuka Lugha zozote hazitakuwa ngumu watanzania kuzitumia. Naujua ugumu nilioupata kujua niyajuwayo, sitopenda mtoto wa kitanzania apitie niliyoyapitia kupata elimu.

Bwana Moshi nafikiri nimekujibu. Nashukuru kuniuliza hilo, kwani CCM wamekuwa wakimtesa sana Mrema kwa hilo. Najua hata mimi wataanza kutumia hilo kama mtaji wa kunipinga nisiwe rais. Lakini hata Mkapa kiingereza chake ni cha kubabaisha pamoja na kwamba alisomea lugha ya kiingereza kama somo ili aweze kuwa mhariri wa DAILY NEWS. Kwa mtaji wa lugha tena ya kiingereza hapa wamefika. Watafute jingine. Ikulu nitaingia tu. Nia na sababu ninazo. Kama walifikiria kwamba uwezo ni kiingereza, basi hata uwezo ninao.  

Kuhusu swali la uraia, maoni yangu ni kwamba Mtanzania anayetaka kurudi kuuchukua uraia wake, itabidi aukane uraia aliouchukua ugenini. Ni maoni yangu binafsi. Lakini kwa sababu tutabadili katiba, sijui maoni ya watanzania yatakuwaje kuhusu hilo. Kulingana na katiba ya sasa, Rais anakuwa kila kitu. Ndiyo maana maswali kama utafanyaje kuhusu hili na lile yanajitokeza kwa wingi. Lakini KATIBA MPYA mambo hayatakuwa hivyo. Kila jambo litashughulikiwa na wizara husika na wanataaluma husika.

Swali la uraia litashughulikiwa idara ya uhamiaji. Katiba mpya itawatengenezea mazingara mazuri ya kufanya kazi yao bila kuingiliwa kisiasa. Kwanza kutakuwa hakuna chama cha kisiasa madarakani.

Maswali mengi niliyatarajia, na bado nayatarajia. Wengi wamezoea sana utawala wa CCM wala hawajui itakuwaje bila CCM. Mimi naiona Tanzania mpya bila CCM. Picha hiyo iko akilini mwangu. Niko tayari kuendelea kuwafafanulia zaidi picha ya Tanzania mpya. Naiona iko nami. Mungu ameiweka maishani mwangu. Hakuna kitakachonitenga na Tanzania mpya iliyo maishani mwangu, labda maisha yenyewe ndiyo yanaweza kunitenga na Tanzania mpya na katiba mpya, halafu MAISHA MAPYA YA WATANZANIA.
Mungu bariki watanzania. Waonyeshe Tanzania mpya bila CCM.


 

Jiandikishe Hapa
Hata kuishi Amerika ni haki yako

 

 
| http://munishi.com |