Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 




TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com

Kibaki ajenga Hospitali ya kisasa Nairobi

Dr. Dan Gikonyo na mkewe Betty, mbele ya hospitali ya kisasa iliyojengwa katika mtaa wa Karen Nairobi. Dr. Gikonyo ni daktari binafsi wa Rais wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki. Hospitali hiyo yenye mitambo ya kisasa, inasadikiwa kuwa ya kipekee Afrika. Inaweza kufanya mambo mengi ambayo viongozi wa Afrika hulazimika kwenda ngambo kutibiwa. Kwamba Kibaki alifikiria kujenga hospitali kama hiyo Kenya, ni hatua inayostahili kupongezwa. Lakini gharama za matibabu katika hospitali hiyo ni za juu kiasi kwamba matajiri tu ndio watakaoweza kumudu. Itambidi Kibaki afikirie jinsi ya kuiboresha hospitali ya Kenyatta ambayo ndiyo hospitali ya rufaa nchini Kenya ili wananchi wa kawaida waweze kumudu gharama za matibabu. Vinginevyo itaonekana kwamba matajiri pekee ndio wanaostahili kuishi Kenya, na wengine wapotelee mbali.

Mitambo ya kisasa ndani ya hospitali mpya ya Kibaki. Kupimwa shinikizo la damu kisha ulazwe hapo wiki moja, ujue shamba na gari pamoja na akiba yako yote imekwisha. Omba Mungu azidi kukulinda na akupe afya njema kwani huwezi kumudu gharama za hapa. Ila pia jifariji kwamba hata hao wenye uwezo wa kutibiwa hapo, hufika mahali mitambo hiyo ikashindwa kuwasaidia na ikifikia hapo inawabidi wakubali kwamba Mungu pekee ndiye anayeweza kulinda afya zetu. Siyo vibaya wenye pesa wakijaribu bahati ya kujiweka hai wazifurahie pesa zao ulimwenguni. Lakini kwa muda gani?


Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais Tanzania Mzee Kawawa akielekezwa kwenye Wadi kulazwa. (Lakini siyo katika Hospitali mpya ya Kibaki , bali Muhimbili Dar es Salaam. Pengine wajifunze kwa Kibaki waboreshe Muhimbili ifikie kiwango cha hospitali ya Kibaki Nairobi) Inasemekana anasumbuliwa na mifupa. Yeye na Nyerere ndio waasisi wa siasa ya Ujamaa Tanzania. Inasemekana Kawawa katika kuitekeleza siasa ya Ujamaa, alisababisha vifo vya mamia ya Watanzania pale alipowahamisha makwao na kuwapeleka msituni ambapo vijiji vya Ujamaa vilitarajiwa kujengwa.Watanzania wengi wakati huo walipoteza maisha yao kwa kuliwa na wanyama pori. Na wengi walikufa kwa njaa pamoja na magonjwa yaliyosababishwa na kurundikwa mahali pamoja msituni bila maji wala matibabu.


 

 
| http://munishi.com |
 
ss