Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 




TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com

Ajali ya Kutisha

Moja kati ya ajali mbaya Tanzania
Ilitokea mchana maeneo ya CHAMAKWEZA katikati ya Mlandizi na Chalinze mkoa wa Pwani nchini Tanzania Afrika ya mashariki. Ilikuwa ni baada ya basi kugongana na magari matatu.Watu 17 walipoteza maisha yao, 14 walikufa papo hapo na wengine walikufa wakiwa njiani kuelekea hospitali. Sita kati ya waliokufa walikuwa kutoka familia moja. Walikuwa wakisafiri kwenye gari aina ya LAND CRUISER iliyokuwa imetokea Singida kuelekea Dar. Hayo ni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Bwana Ally Mbilikila.Watu 24 walijeruhiwa vibaya, jambo linaloashiria kwamba idadi ya waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo kuongeeka. Imetajwa kama ajali mbaya kuwahi kutokea Tanzania. Ilihusisha magari manne, likiwemo basi la abiria "JVC." Pia iliarifiwa kwamba watu wa kwanza kuwasili maeneo ya ajali, walijihusisha na kuwapora majeruhi pamoja na wale waliopoteza maisha.Walionekana wakiwasachi mifukoni na kuchukua kila walichokipata. Iwe ni simu za kiunga mbali, au pesa pamoja na mabegi ya kusafiria, vyote viliishia mikononi mwa wezi hao. Mmoja kati ya majeruhi alisikika akisema kwamba badala wamsaidie kutoka katika mabaki ya Basi lililohusika kwenye ajali, wao walikuwa wakimpekua mifukoni bila ya huruma. Dereva wa Lori alikufa papo hapo na hajatambulikana. Pia kwenye sakata hilo la ajali , ilikuwepo LAND CRUISER nyingine inayomilikiwa na wizara ya ujenzi. Kilichosababisha ajali hiyo bado ni kitendawili. Basi la abiria kugongana na magari matatu hiyo ni ya aina yake.


"Je Ubinadamu uko wapi? Simu Pesa na Mabegi ya kusafiria yamekuwa muhimu kuliko maisha ya watu? Aibu kubwa kwa watanzania waliofanya kitendo hicho."

Watatu waponea chupuchupu

Hawa jamaa watatu wa asili ya kieshia wameponea chupuchupu baada ya gari lao kukosa njia na kugonga nguzo ya umeme. Ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya Ngong sehemu ya Lenana asubuhi ya tarehe 2/.7/2005. Abiria wawili pamoja na dereva walifanikiwa kutoka bila majeraha yeyote, lakini gari lao liliungua nyanga nyanga. Tofauti na vibaka wa Tanzania waliowapora majeruhi, Wakenya waliofika sehemu ya ajali walionekana kuwasaidia waeshia ambao walikuwa na kiwewe pamoja na kuchanganyikiwa.


45 walipuliwa London

Watu 45 wameripotiwa kufa huku wengine 700 wakijeruhiwa vibaya mjini London baada mabomu kulipuka sehemu mbali mbali nchini Uingereza Alhamisi ya tarehe 7/7/2005. Kundi la Alkhaida linaloongozwa na Osama Bin Laden limedai kuhusika na milipuko hiyo, Katika taarifa waliyoitoa kupitia Mtandao wa kompyuta duniani. Taarifa hiyo ilisema kwamba wamelazimika kulipua London ili kulipiza kisasi mauaji ya maelfu ya raia wa Irak yanayotekelezwa na majeshi ya uingereza, ambayo kwa sasa yako nchini Irak. Taarifa hiyo pia iliongeza kusema kwamba mashambulizi zaidi yako njiani endapo Amerika na Uingereza hazitaondoa majeshi yake Irak. Nae waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair aliropoka kwamba Waislamu ndio walioishambulia London. Matamshi yake yamezusha hofu kubwa kwa waislamu nchini Uingereza ambao sasa wanaitaka serikali ya Blair kuwalinda kutoka mashambulizi ya wakristo watakaoamua kulipiza kisasi. Walimlaumu Brair na Bush wa Marekani kwa sera zao mbovu kuwahusu waislamu, ambazo ndizo zinazochochea mashambulizi ya kila mara na maisha ya watu wasio na hatia kupotea. Walimtaka Brair ajilaumu mwenyewe kabla hajaanza kuwalaumu Waislamu. Walionya kwamba endapo Amerika na Uingereza hawataacha kuwakandamiza Waislamu, basi mashambulizi kama haya hayatakoma duniani. Wadadisi wa mambo wanasema kwamba Tangu Amerika iamue kuishambulia Irak kwa kile ilichokiita kumaliza ughaidi duniani, mambo yamekuwa kinyume chake. Badala ya ughaidi kumalizika, inaonekana kwamba hatua ya Marekani imechangia kuongeza ughaidi badala ya kuupunguza. Kwamba maghaidi wanaweza kuishambulia London asubuhi na kuharibu sekta ya usafiri kabisa, hiyo inaonyesha kwamba maghaidi wanaweza kushambulia popote na wakati wowote. Kwa sasa London wanajifariji kwamba walijua itatokea. Swali wengi wanalouliza ni kwamba kama walijua, mbona hawakuzuia?

Unasemaje?/ Tuandikie

Full Name
E-mail
Subject
Message
   
   

 

 
| http://munishi.com |